ZIARA ya Rais wa TFF Jamal malinzi hatimaye imemelizika leo hapa jijini Mwanza kwa matukio mawili makubwa kufanyika.
Tukio la Kwanza limefanyika majira ya saa 2:30 katika ofisi za Halmashauri ya jiji la Mwanza ambapo Shirikisho hilo limesaini mkataba kati yake na Halmashauri hiyo kwaajili ya kuboresha uwanja wa Nyamagana.
Ili ipate kumwaga fedha zake za msaada kiasi cha dola laki 5 ambapo nyingine dola laki 1 zitatoka Halmashauri ya jiji la Mwanza, FIFA ilikuwa ikitaka uthibitisho toka TFF kuwa uwanja huo kwa miaka yote utatumika kwa matumizi ya michezo yaani soka na si vinginevyo kwaajili ya kuanza uboreshaji wa uwanja huo uliokuwa na utata wa kutaka kubadilishwa matumizi.
Tukio la pili Malinzi na timu yake ya wataalamu toka TFF, majira ya saa 4 asubuhi imetembelea na kukikagua kituo cha elimu na soka cha Alliance Academy ikiwa ni mwanzo wa mpango wa kitaifa wa kuwekeza katika soka la vijana.
Jamal
Malinzi alipata fursa ya kuzungumza na wachezaji na wanafunzi vijana
wanaochukua masomo ya usimamizi na uamuzi wa michezo (marefa), kikubwa
sanjari na kuzingatia michezo pia alisisitiza kuiweka elimu mbele.
|
Kumbe TFF mnao uwezo wa kukarabati viwanja sasa mbona hamkarabati viwanja vya mpira vya serikali kama nyamagana? na kuachana na viwanja vya binafsi!
ReplyDeleteMdau wa kwanza, hujui kwamba wameshasaini mkataba kati ya manispaa ya jiji la mwanza na TFF Ili kuukarabati na kuwekea nyasi bandia chini ya ufadhili wa FIFA wa dola 500000? jiji la mwanza limeshachangia dola 100,000.
ReplyDeletekazi nzuri
ReplyDeleteFanya kazi Malinzi....onesha tofauti...
ReplyDelete