Mkurugenzi wa Kampuni ya Saseni Media, Bw. Issa Mbura akizungumza katika warsha hiyo kwa wasanii mbali mbali wa filamu hapa nchini.
Kampuni ya Saseni Media, kwa kupitia mpango wake wa kukuza vipaji vipya vya uigizaji na kuvisimamia, iliendesha kwa mafanikio makubwa zoezi la usaili kwa waigizaji wazoefu na wanaochipukia siku ya jumamosi, tar 25 Januari 2014.
Idadi kubwa ya watu ilijitokeza kujisajili na kufanyiwa usaili na kila mwigizaji alionekana kuwa ni mwenye shauku ya kutaka kupata fursa hiyo na hivyo kuonyesha umahiri wake katika uigizaji. Akizungumzia usaili huo, Mkurugenzi wa Kampuni ya Saseni Media, Bw. Issa Mbura amesema
“Zoezi lilienda vizuri na pamoja na kupata vipaji kama lilivyokuwa kusudio letu, pia tumeshuhudia mambo kadhaa yakijitokeza kama changamoto kwa tasnia ya filamu inayotegemea sana waigizaji ili kufanya vizuri,”
“Moja, ni kwamba Tanzania kuna waigizaji wengi wanaochipukia na kutafuta fursa za kuigiza kuliko wale wachache tuliozoea kuwaona kwenye luninga zetu,”anasema Mwl. Issa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...