Mchezaji wa Timu za Dacico Pooltable, Yohana Mathius, akijaribu kulenga shimo wakati wa mchezo wa kirafiki dhidi ya Mlimani Profesional Pooltable katika hafla ya Sherehe za kuwakaribisha wanafunzi wapya wa Dar es Salaam City College na Mlimani Profesional(School Bush) iliyofanyika kwenye ukumbi wa Chuo cha Dar es Salaam City College Kibamba jijini Dar es Salaam Jana.
Wanafunzi wa Chuo cha Uandishi wa Habari na Utawala Dar es Salaam City College, wakati wa wakati wa kutafuta washindi wa Urembo Miss & Mr. Dacico kwenye Hafla ya kuwakaribisha wanafunzi wapya wa Vyuo vya DACICO na Mlimani Profesional, iliyofanyika Makao makuu ya Chuo cha DACICO kibamba Chama jana na kushirikisha michezo mbali mbali ikiwamo Soka, Pooltable, kuimba, kucheza muziki, kuogelea, Urembo Mr. & Miss New Intake DACICO na mashindano ya kujibu Mada(Debate).
Wachezaji wa Timu za Dacico Fc, kiungo Machejo Dula (nyekundu) na mlinzi wa timu ya Mlimani Profesional Fc. Masanga Mkama wakiwania mpira wakati wa mchezo wa kirafiki katika hafla ya Sherehe za kuwakaribisha wanafunzi wapya wa Dar es Salaam City College na Mlimani Profesional(School Bush) iliyofanyika kwenye Viwanja vya Kibamba Chama, jijini Dar es Salaam Jana. hadi mwisho wa mchezo Dacico iliibuka na ushindi wa bao 1-0.





Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...