Sehemu ya Vikosi vya Ulinzi na Usalama vilivyoshiriki kwenye Sherehe za Maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar,yanayoendelelea kufanyika hivi sasa kwenye uwanja wa Amani,Zanzibar leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Ali Mohamed Shein akikagua gwaride la heshima wakati wa kilele cha sherehe za miaka 50 ya Mapoinduzi ya Zanzibar katika uwanja wa Amani Abeid Karume leo January 12, 2014.
Vijana wakiachia njiwa kama alama ya amani wakati wa kilele cha sherehe za miaka 50 ya Mapoinduzi ya Zanzibar katika uwanja wa Amani Abeid Karume leo January 12, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Ali Mohamed Shein wakimpongeza Rais Yoweri Kaguta Museveni aliyeongea machache wakati wa kilele cha sherehe za miaka 50 ya Mapoinduzi ya Zanzibar katika uwanja wa Amani Abeid Karume leo January 12, 2014
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Ali Mohamed Shein kwa hotuba nzuri aliyotoa wakati wa kilele cha sherehe za miaka 50 ya Mapoinduzi ya Zanzibar katika uwanja wa Amani Abeid Karume leo January 12, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Yoweri Kaguta Museveni wakiongea wakati wa kilele cha sherehe za miaka 50 ya Mapoinduzi ya Zanzibar katika uwanja wa Amani Abeid Karume leo January 12, 2014. PICHA NA IKULU.

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Kuna story inaendelea kuwa kesho ni mapumziko, ni kweli.

    ReplyDelete
  2. Imependeza sana, nimeona wapanda 'Vespa' nao hawakuwa nyuma, next time tusiwasahau na wasukuma 'marikwama' pamoja na waendesha baskeli ndio jumla ya wana Mapinduzi Visiwani Zanzibar.

    ReplyDelete
  3. hapo museveni anaponyoosha mikono yote nani anaweza kutabiri amemwambia nini kikwete? (a) __ (b)-- n.k. n.k

    ReplyDelete
  4. hapo museveni anasema kuwa atatawala EA yote, ndio maana kainua mikono yote juu

    ReplyDelete
  5. Mdau wa 4 huyo M7 atatawala Afrika ya Mashariki yote akiwa na umri gani tena?

    Wakati yeye sasa ana umri wa miaka 86 sawa na mwaka alioingia Madarakani mwaka 1986?

    Je, atairudisha miaka ya Kalenda nyuma?

    Wakati yeye na Marehemu Nelson Rolihlahla Mandela wamepisha kidogo tu?

    Au atafoji vyeti vya kuzaliwa na kushusha umri chini ili agombee Uraisi wa EAC?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...