1Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Nyumba nchini (NHC), Bw. Nehemia Kyando Mchechu akizungumza wakati wa maadalizi ya ufungaji wa mafunzo ya vijana wawakilishi wa vikundi kutoka mikoa mbalimbali kuhusu utengenezaji wa matofali ya udongo yenye teknolojia ya Interlocking Blocks yaliyoanza Januari 6 mpaka 17 mwaka huu ambayo yanatarajiwa kufungwa wiki ijayo na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda, Mkurugenzi huyo amesema Shirika la nyumba badala ya kwenda kutoa msaada wa sabuni na vyakula katika vituo vya watoto yatima au kusaidia biskuti limeamua kubadilisha maisha ya vijana wa Tanzania kwa kuwapa mafunzo na kuwapatia mashine za kutengeneza matofali ya udongo ambayo wao NHC watakuwa ndiyo wateja wakuu wa kununa matofali hayo, lakini pia shirika hilo linatoa mashine za kufyatulia matofali zipatazo 640 katika wilaya 160 mikoa yote ya Tanzania bara na kiasi cha shilingi 500,000 kila mkoa kama mtaji wa kununulia saruji kwa vikundi hivyo, Katikati ni Injinia Kwanama Elias Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo kutoka Nation Housing&Building Research Agency (NHBRA) na kushoto ni Bw.Julius Njelwa kutoka VETA, mafunzo hayo yameratibiwa kwa pamoja na (NHC), (VETA) na (NHBRA) kwa pamoja.3 Injinia Kwanama Elias Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo kutoka Nation Housing&Building Research Agency (NHBRA) akifafanua masuala ya kitaalamu kuhusu teknolojia hiyo ya matofali kwa waandishi wa habari. 4Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo. 7Baadhi ya maofisa wa Shirika la Nyumba NHC wakiwa katika maadalizi hayo kushoto ni Suzan Omary Meneja Mawasiliano NHC, Muungano Saguya Meneja huduma kwa jamii NHC na Ephraim Kibonde mtangazaji wa Clouds Radio.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Doris ChandoJanuary 17, 2014

    ni habari nzuri, shirika la nyumba mnastahili hongera kwa hili

    ReplyDelete

  2. kabwe rudi nymbani, ukitoka GEREZANI, uje ujiunge nasi, kilijenga taifa kabwe.

    ReplyDelete
  3. Jamani huyu dada Ms Omary ni mtu mzuri na mchpa kazi sana! Mungu Ibariki Tanzania!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...