Pichani kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Masuala ya Kimataifa wa Shirika la Posta Tanzania,Bwa. Elia Madules akizungumza mbele ya Wanahabari (hawapo pichani),mwishoni mwa wiki ndani ya Ofisi ya Makao Makuu wa ya shirika hilo jijini Dar,kuhusiana na maadhimisho ya miaka 34 ya siku ya Posta Barani Afrika,Siku ambayo Posta zote katika Afrika hufanya maadhmisho yanayohusu shughuli za Kiposta,Pichani kati ni Kaimu Meneja Mkuu Uendeshaji Biashara,Bi.Fadya Zam pamoja na Kaimu Meneja Mipango Bwa.Nehemiah Kyabalasi
Pichani kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Masuala ya Kimataifa wa Shirika la Posta Tanzania,Bwa. Elia Madules akifafanua jambo kwa ufasaha mbele ya Wanahabari (hawapo pichani),mwishoni mwa wiki ndani ya Ofisi ya Makao Makuu wa ya shirika hilo jijini Dar,kuhusiana na maadhimisho ya miaka 34 ya siku ya Posta Barani Afrika,Siku ambayo Posta zote katika Afrika hufanya maadhmisho yanayohusu shughuli za Kiposta.Bwa.Elia alisema kuwa dhamira ya Shirika hilo ni kuhakikisha kuwa Watanzania wanafaidika na matunda ya huduma bora na za kisasa za mawasiliano ya Posta ambayo ni pamoja na kuwarahisishia upatikanaji wa huduma za kibiashara na kupanua wigo wa huduma jumuishi za kifedha
Pichani kati ni Kaimu Meneja Mkuu Uendeshaji Biashara,Bi.Fadya Zam akifafanua zaidi kuhusiana na maadhimisho hayo ya miaka 34 ya siku ya Posta Barani Afrika Mbele ya Wanahabari (hawapo pichani),Siku ambayo Posta zote katika Afrika hufanya maadhmisho yanayohusu shughuli za Kiposta,Bi Fadya aliongeza kuwa siku hiyo ni Kumbukumbu ya kuanzishwa kwa umoja wa Posta Barani Afrika (PAPU) mnamo tarehe 18 Januari 1980,akabainisha kuwa hivyo Umoja huo ambao ni Shirika tanzu la Umoja wa Afrika (AU) umetimiza miaka 34.Bi Fadya alisema kuwa hivi sasa PAPU ina nchi Wanachama 43 na Tanzania ndio mwenyeji wa makao yake Makuu yaliyoko jijiini Arusha.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Shirika hilo la Posta Tanzania,wakifuatilia mkutano huo uliohusu maadhimisho hayo ya miaka 34 ya siku ya Posta Barani Afrika.
Pichani Kulia aliyesimama ni Mkuu wa Uhusiano Shirika la Posta Tanzania,Bwa.Wilfred Mlugo akitoa muongozo kwenye mkutano huo.
Pichani kulia ni Kaimu Meneja Mipango,Bwa.Nehemiah Kyabalasi akielezea mipango mbalimbali ya Shirika hilo kwa Wanahabari (hawapo pichani).Bwa.Nehemiah alieleza kuwa maadhimisho hayo yanafanyika wakati shirika la posta limetimiza miaka 20 tangu kuanzishwa kwake mnamo tarehe 1 januari,1994,ambapo tangu wakati huo yamekuwepo mafanikio ya kuridhisha lakini pia changamoto za hapa na pale hazikosi.
MBANA SHIRIKA LA POSTA LIMEANZA KUFANYA KAZI ZA UAJENTI WA BENKI NYINGINE? INAELEKEA MAMBO YA UIUA BENKI YA POSTA YANAKUJA KWA MLANGO WA UANI.
ReplyDelete