Familia ya Marehemu Samson Francis Marunda Woiso wanatoa shukrani zao za moyoni kwa ndugu, jamaa, marafiki, majirani na wanajumuiya wa Mtakatifu Martha and Muungano wa Jumuiya nne, kwa kuwa pamoja nasi na kutufariji wakati wa msiba na mazishi ya mpendwa wetu Samson Francis Marunda Woiso aliyetwaliwa na Bwana tarehe 13 December 2013 katika hospitali ya Huruma, Rombo na kuzikwa tarehe 17 December 2013 nyumbani kwake Nanjara-Urauri, Rombo. Jinsi mlivyoguswa na kuomboleza msiba huu, ushirikiano wenu mkubwa na michango yenu sio tu ilitusaidia sana katika kufanikisha huduma zote za kumlaza mahali pake pa milele Baba yetu mpendwa, Mzee Woiso bali pia ilitupa nguvu ya kupokea kifo cha mpendwa wetu!
Tunatoa shukrani za kipekee ziwafikie watumishi wa kiroho hasa Paroko Protas Swai wa Kanisa la Roho Mtakatifu, Reha, Padri Genes Mahedi, Paroko Msaidizi wa Parokia ya Damu Takatifu ya Yesu, Tegeta, na Wachungaji wa KKKT Mmanga (Usharika wa Uswaa), James Nkya (Usharika wa Majengo) na Fred Njama (Usharika wa Karanga Soweto).
Ni vigumu kumshukuru kila mtu mmoja mmoja kwa majina yao, hivyo tunaomba kwa moyo mkunjufu kila mmoja apokee shukrani zetu za dhati kwa misaada yenu mlioitoa katika kipindi chote cha msiba. Tungependa kutoa shukrani za dhati kwa Jumuiya ya Mtakatifu Martha (Parokia ya Reha); Muungano wa Jumuiya nne ya Mtakatifu Christogone (Parokia ya Reha); Wafanyakazi wa NMB; NBC Mlimani City; Kiliwater Company Limited, Mkuu, Rombo; G32-KNCI JVE Limited; Umoja wa Umata, Rombo; Tarakea Rural Cooperative Society Limited; Kilimanjaro Cooperative Bank; WIOMSA; Department of Aquatic Sciences and Fisheries, Department of Zoology and Wildlife Conservation na Institute of Marine Sciences (University of Dar es Salaam). Vile vile tunawashukuru sana Kikundi Wazee Wastaafu, Tarakea and Wanachama wa Kikundi cha MIBS.
Na mwisho ni wote walioshirikiana nasi kwa kutufariji na kuomboleza nasi kwa njia moja au nyingine. Wote tunawaombea Mwenyezi Mungu awaongezee na kuwabariki!
Tunawaomba nyote muungane nasi katika kumuombea marehemu apate punziko la milele.
MUNGU AMETOA, MUNGU AMETWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE!
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...