![]() |
| Marehemu Jane Lillian Samatta |
Familia ya Mh. Jaji Mkuu Mstaafu Barnabas A.
Samatta inatoa shukrani zetu za dhati kwa wale wote walioshiriki kwa namna moja
au nyingine, katika kuwafariji katika msiba wa mpendwa wao, Jane Lilian
Samatta, aliyefariki tarehe 09 Disemba, 2013, katika Hospitali ya TMJ hapa Dar
Es Salaam.
Shukrani za kipekee ziwafike wafuatao: Mh.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed Chande Othman; Mh. Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu; Waheshimiwa
Majaji wa Mahakama kuu ya rufaa na wa Mahakama kuu; Waheshimiwa Majaji Wastaafu;
Mtawala Mkuu wa Mahakama Bw. Hussen Kattanga; Waziri wa mambo ya nje na
ushirikiano wa kimataifa Mh. Bernard Membe; Prof. Mkude, Mwenyekiti wa Baraza
la Chuo Kikuu Mzumbe; Prof. Joseph Kuzilwa, Makamu Mkuu wa Chuo na Makamu wake,
Prof. F. Kamuzora na Prof. J.S. Itika, na jumuia ya chuo Kikuu hicho cha
Mzumbe.
Mh. Makamu Mwenyekiti wa Judges and Magistrates Vetting Board ya
Kenya
Bi. Roseline Odede, Mh. Mjumbe na Mtendaji
Mkuu wa Bodi hiyo, Waheshimiwa Justus Munyithya na Reuben Chirchir, pamoja na Viongozi
wengine na Watumishi wa Bodi hiyo;
Meneja
Mkuu wa Kampuni ya Sigara Tanzania (TCC) Bw. Abdo Majd, Viongozi na Watumishi
wote; Menejimenti na Watumishi wa Management
And Development For Hearth (MDH);
Walimu na Watumishi wa Shule ya Msingi ya
Libermann; Madaktari na Wauguzi wa Hospitali ya TMJ; Dr. Mwandolela, Dr. Paschal
na Wauguzi wa Heameda Medical Clinic;
Majirani wa Mtaa wa Bongoyo na Mitaa ya jirani; Majirani wa Oyster Bay Neighborhood Association (CONA);
Vikundi vya Green Women na Great Sisters;
Wanajumuia wa Jumuia ya Mtakatifu Agostino wa Hippo; Bi. Eliaebeth Mwella; Bw.
Aaron Tesha; Bi. Diana Mkapa; Bi. Magdalena Ingi; Bi. Gloria Sindano; Viongozi,
Kwaya ya Kanisa na Waumini Kanisa Kuu la Mtakatifu Albano; Ndugu, Jamaa na
Marafiki.
IBADA YA SHUKRANI
Itafanyika
katika kanisa kuu la mtakatifu Albano jijini Dar es salaam kesho Jumamosi saa 2 asubuhi tarehe 11 January 2014.
MPENDWA WETU JANE, MIKONONI
MWA MWENYEZI MUNGU PUMZIKA,
MIOYONI MWETU ISHI DAIMA.



RIP Dada Jane, Missing u so much!
ReplyDeleteR.I.P Jane!
ReplyDeleteSoo beautiful yet gone, Rest in Peace Jane.
ReplyDeleteOur collective hearts are heavy with over Jane's death. She was such a great person,gone too soon. Lets her live on in our memories forever.
ReplyDeleteRest In Peace Jane...
ReplyDeletePoleni sana Familia ya Rt Jugde Samatta - she has gone too soon... Tulikuwa pamoja enzi Za kusoma Tabora!
Mwenyenzi Mungu mwingi wa rehema awape faraja na ustahmilivu katka kipindi hiki kigumu sana kwenu!
Bwana alitoa na bwana ametwaa - Jina lake lihimidiwe.
Aisee naona familia ya Mheshimiwa imekuwa kwenye kipindi kigumu ukizingatia muda si mrefu ulopita mliondokewa na kijana wenu mpendwa.
ReplyDeleteMungu awape nguvu kipindi hiki kigumu...Dunia ni mapito
RIP
R.I.P Jane....
ReplyDelete