Gazeti la Tanzania Daima la tarehe 23 Januari, 2013 liliandika makala inayosomeka "JK AMNUSURU MFUNGWA WA ERA". Gazeti hilo lilidai mfungwa wa kesi ya ERA Ajay Somani ametolewa gerezani kwa njia ya kutatanisha wakati wafungwa wengine waliokuwa kesi moja wanaendelea kusota gerezani.
Maelezo mafupi kuhusu suala hilo ni kwamba mfungwa Na. 74/2012 Ajay Suryakant Somani tarehe 22 Novemba, 2012 alihukumiwa kifungo cha miaka miwili na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu shauri la Jinai Na. 1164/2008 kwa kosa la "Obtaining Money by False Pretence c/s 302 of the Penal Code".
Watuhumiwa wenzake katika kesi hiyo walikuwa Sophia Joseph Lalika, Ester Komu na Emmanuel Mwakyosa. Hawa walikuwa wanakabiliwa na shtaka la "Occasioning Loss to a Specified Authority". Hawa walihukumiwa kifungo cha miaka mitatu au faini shilling! milioni tano (Tzs.5,000,000/=) kila mmoja. Wafungwa wawili Ester Komu na Emmanuel Mwakyosa walilipa faini siku hiyo hiyo mahakamani na kuachiliwa huru. Mfungwa Sophia Joseph Lalika kwa kuwa hakulipa faini hiyo mahakamani alipelekwa gerezani na tarehe 23/11/2012 alilipa faini hiyo na kuachiliwa huru. Hivyo madai yaliyotolewa kwamba bado wanasota gerezani siyo ya kweli.
Kuhusu Mfungwa Na. 74/2012 Ajay Suryakant Somani wakati akiendelea na kifungo chake gerezani alipata mapunguzo ya 1/6 ya kifungo chake kwa msamaha wa Rais uliotolewa kwa wafungwa tarehe 9 Desemba, 2013 wakati wa kuadhimisha miaka 52 ya Uhuru wa nchi yetu. Mapunguzo haya ya 1/6 ni zaidi ya mapunguzo ya kawaida 1/3 yanayotolewa chini ya Sheria ya Magereza ya mwaka 1967. Kutokana na msamaha huo kifungo chake kupunguzwa kwa nusu (1/3 + 1/6 = 1/2) yaani mwaka mmoja na kwa hali hiyo kustahili kuachiliwa huru tarehe 9/12/2013.
Wafungwa wengine waliotajwa No.247/2011 Farijala Shabani anayetumikia kifungo cha miaka kumi na moja (11) na Na. 345/2011 Rajabu Maranda anayetumikia kifungo cha miaka kumi (10) nao walinufaika na msamaha huo wa Mhe. Rais lakini waliendelea kubaki gerezani kutokana na urefu wa vifungo vyao.
Hivyo Gazeti husika lifute kauli hiyo kwa kuwa waliachiliwa huru kwa mujibu wa sheria na kwa sasa ni raia huru.

John C. Minja 
KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA

23 Januari, 2014

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Nafikiri makosa ya wizi wa mali ya umma hasiwe na msamaha!!

    ReplyDelete
  2. Kwa nini Tz inachukulia makosa ya EPA kama makosa ya kawaida.? Mbona huu NI UHUJUMU UCHUMI.Nadhani,si mbali ,itabidi turevew makesi mengi kama haya,na tuongeze watuhumiwa.Wanajijua,wajitayarishe aisee!

    ReplyDelete
  3. asanteni Tanzania daima, Keep up informing us. Kamata kamata ya EPA na hukumu zake zilikuwa ni mchezo wa kuigiza. Fisadi kaiba TZS 10 billion, anafungwa kifungo cha miaka 11 bila ya kutakiwa kuzirudisha pesa hizo alizoiba. Akitoka kifungoni nakuwa huru kuzifukua pesa hizo na kula bata kilaini bila kudaiwa tena. Mbaya zaidi baada ya miaka 2-3 anapata msamaha wa raisi. Hii itaongeza wananchi kukosa imani na vyombo vya dola. AlexBura dar

    ReplyDelete
  4. Vyombo vyetu vya habari havina umakini kabisa. This is a serious national challenge! Hawa ndio tunawatarajia kuutaarifu umma? Hivi walishindwa kumpigia msemaji wa Idara husika?

    ReplyDelete
  5. Wandugu,

    Kulingana na Mchezo wa ulaji unavyo kuwa ni kwamba hiyo hela anakuwa mara zingine haja fanya Hujuma kwa gemu moja.

    Anakuwa anakula muda baada ya muda huku akishirikiana na wengine!,,,kama ujuavyo ktk laji lazima wengine watachomoka na wengine kuliwa kafara hivyo atakaye liwa kafara ndiye atakaye pigiwa hesabu yooote ya hasara na kukuta Mabilini ya Shilingi, sioyo ktk Gemu moja inakuwa kwa muda mrefu wizi unafanyika.

    Mkitaka muamini hicho kitu ni huyo mama mmoja Sophia Lalika yeye hakuwa na kitu hapo (Shs. 5 Millioni za Faini) ikabidi aende Lupango na ndipo ndugu zake nje wajikusanye ili Bi Mkubwa atoke Mukenge!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...