Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania – TRL unawatangazia abiria wote na wananchi kwa jumla kuwa kutokana na sababu za kiufundi unasikitika kuwa treni ya abiria iliyopangwa kuondoka leo Jumanne Januari 07, 2014 saa 3 usiku kwenda bara imeahirishwa hadi keshokuwa siku ya Alhamis Januari 09, 2014, saa 3 usiku.

 Taarifa hiyo imefafanua kuwa dharura hiyo ya kuahirisha safari imetokana na ajali ya treni ya mizigo iliyotokea juzi saa 2 usiku kati ya Stesheni za Luiche na Kigoma na kusababisha treni ya abiria kutoka Kigoma kushindwa kuondoka kuja Dar. 

 Wakati huo huo taarifa iiliyopatikana mchana huu imethibitisha kuwa ukarabati wa eneo lililoathirika na ajali ya treni ya mzigo ya juzi umekamilika na njia imefunguliwa saa 8:45 mchana huu. Aidha treni ya abiria kutoka Kigoma kuja Dar imeshaondoka mjini Kigoma tokea saa 9:20 alasiri ya leo. 

 Aidha taarifa hii iwafikie wadau wote wa usafiri na huduma ya reli ya kati na kwamba uongozi wa TRL unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.

 Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji 
 Mhandisi Kipallo Amani Kisamfu. 
 TRL Makao Makuu, 
 Dar es Salaam. 
 Januari 07, 2014

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Ankal,

    Asala-maleko!

    Taswira hii nzui ni stesheni gani Tanzania.

    Maana treni na mandhari ya mlima kwa mbali picha yavutia kweli kweli.

    Mdau
    Globu ya Jamii

    ReplyDelete
  2. Nchi kubwa kama Tanzania ina treni moja tu. Ama kweli sisi ni masikini!!

    ReplyDelete
  3. Mdau wa pili, unaishi wapi kweli? siku zote hukujua kuwa Tren ni moja na njia ni moja? upo kweli Tanzania au upo nchi za watu? Tanzania ni maskini kwa ujumla wake

    ReplyDelete
  4. HAPA NI MOROGORO NA NYUMA NI MILIMA YA URUGURU.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...