Marehemu Kepteni Sam Chekingo
Habari zimetufikia punde kwamba rubani wa ndege maarufu nchini Kepteni Sam Chekingo amefariki dunia Jumanne asubuhi nyumbani kwake Kinondoni jijini Dar es salaam. Kwa mujibu wa rafiki wa karibu wa marehemu Balozi Cisco Mtiro, misa ya kumuombea marehemu itaanza saa nne asubuhi Ijumaa ynyumbani kwake, kabla ya mwili wake kupelekwa katika makaburi ya Kinondoni saa tisa alasiri siku ya Ijumaa (sio Leo, kunradhi)
Marehemu Kepteni Chekingo atakumbukwa kama mmoja wa marubani mahiri na wa muda mrefu wa ndege za serikali alikotumikia toka enzi za Rais wa awamu ya kwanza hayati Mwalimu Nyerere. Alistaafu kazi serikalini na kujiunga na Umoja wa Mataifa akifanyia kazi zake Congo Brazaville, kabla ya kurejea nyumbani na kujiunga na ATC alikofanyia kazi hadi mauti yalipomkuta.
Mola aiweke Roho ya marehemu mahali pema peponi
AMINA



Pole Cindy Chekingo
ReplyDeletePoleni wafiwa.
ReplyDeleteI have lost a very dear friend. Poleni Samson, Brenda, Aron, Babu Cindy, Aidan and Amani.
ReplyDeleteMay his soul rest in piece. Captain Cheking was a great man, a real representation of hard work and zeal.
Hili jina kama si geni...hakuwahi kukaa Ukonga huyu...tumeshazeeka wengine...
ReplyDeleteAnyway RIP Capten
Buriani rafiki yangu Buriani rafiki.
ReplyDeleteNitakumbuka ucheshi wako na mzaha uliokuwa ukipenda.
Capt checks was a friend of everybody.. he was full of love. Poleni sana sam, ronald, brenda, cindy, canaan, andrew.. mungu aendelee kuwatia nguvu. Amin
ReplyDelete