Marehemu Mzee Arnold Wilfred Nkhoma Kambonapany (kulia) enzi za uhai wake akiwa na mmoja wa watoto wake kwenye ibada maalum ya kutoa shukrani alipotimiza miaka 100 iliyofanyika kwenye kanisa la Mtakatifu Andrea Magomeni jijini Dar hivi karibuni.
Familia nzima ya Nkhoma Kambonapany wanasikitika kutangaza kifo cha baba na babu yao mpendwa Mzee Arnold Wilfred Nkhoma Kambonapany, kilichotokea kwenye hospitali ya Mount Ukombozi tarehe 17/01/2014.
Taarifa za msiba ziwafikie Doctors Colin na Nicholas Darch wa Cape Town Afrika Kusini , Bi Laura Amrei wa Hamburg Ujerumani , Bi Ajira Darch wa San Fransisco , California , Marekani , Bwana Monday Wamunza akiwa Maryland , Marekani , ndugu na jamaa popote walipo.
Alijaliwa kupata watoto 11, wajukuu 36 , na vitukuu 25. Msiba unafanyika kwa mtoto wake Professor Alice Wamunza Nkhoma , Nyumba na. 07 , Mtaa wa Koroshoni , Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam.
Maziko yatafanyika tarehe leo 19/01/2014 kwenye makaburi ya Kinondoni.
Msafara wa mazishi utaanzia saa tano za asubuhi chuo kikuu baada ya chakula na kutoa heshima za mwisho.
Baada ya hapo utaelekea Kanisa la Mtakatifu Andrea Magomeni kwa ajili ya Misa.
Baada ya hapo utaelekea Kinondoni makaburini kwa kumpumzisha Mzee Kambonapany.


Loh!Binafsi siifahamu hii familia ya mzee Nkhoma ila napenda kuwapa pole sana wana familia na shukrani kwa kumtunza huyu mzee hadi umri huu.Pumzika kwa amani Mzee Anorld.Kizazi cha hawa wazee kilikuwa kinafahamu kuitunza miili yao kwa vyakula "natural'" na mazoezi ya kutembea kwa miguu kijiji hadi kijiji(miaka 100 siyo mchezo)siyo mambo yetu haya ya kisasa(sitayataja)
ReplyDeleteDavid V
Poleni sana wanafamilia nilifarijika mno kuona sherehe yake ya kutimiza miaka 100 hivi karibuni nadhani ni wiki iliyopita kumbe ndo ilikuwa sherehe yake ya mwisho hapa duniani. Mungu awape faraja wanafamili wote
ReplyDeletePOLENI SANA WANAFAMILIA,NIMESIKITIKA SANA NA KIFO CHA HUYU MZEE KWANI NI WIKI ILIYOPITA NIMEMUONA KWENYE SHEREHE YAKE YA MIAKA 100,SII KAZI RAHISI KUFIKIA HAPO.MWENYEZI MUNGU AKUPE PUMZIKO LA MILELE NA MWISHO UKAPATE KUFUFULIWA NA KRISTO ILI UPATE UZIMA WA MILELE AMENI.
ReplyDeletePoleni sana wanafamilia pamoja na wote wahusikao na msiba huu. Ni siku chache tu hapo nyuma tu siku chache zilizopita nilikuwa nikiangalia picha kadhaa akiwa anasherehekea 'Birthday' yake ya kutimiza miaka 100 kwa Ibada maalum ya kumshkuru Mungu juu ya hilo, leo hii maskini ameitwa na Muumba, nae kaitika wito huo. Poleni sana wanafamilia na wote mlioguswa na msiba huu, Mola awape faraja na moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo ya kuondokewa na mpendwa wetu Mzee Arnold Wilfred Nkhoma. Rest In Peace mzee wetu.
ReplyDeleteR.I.P mzee Anorld
ReplyDeletepoleni sana wanafamilia, nimepokea kwa masikitiko makubwa msiba Mzee NKhoma japo simfahamu, lakini ni majuzi tu nimeona sherehe yake ya kutimiza miaka hapa kwenye GLOBU YA JAMII.Mola ailaze roho yake mahala pema peponi. AMEIN.
ReplyDeleteFamilia nzuri hii, mfano wa kuigwa. Binafsi nimeguswa na huu msiba! Kwani last week tulisheherekea Birthday Kwenye blog sherehe yake ya 100 years! Familia poleni, na Mfarijike Kuwa yuko sehemu bora zaidi! Barikiweni, familia Staarabu !
ReplyDeletePoleni sana Prof. Alice, Agnes na familia nzima ya + Mzee Nkhoma. Apumzike kwa amani. Pia nawashukuru nyie kwa kuwa watoto/wajukuu wazuri wenye upendo wa dhati kwa mzazi wenu maana mgekuwa mnampa presha baba yenu asingefikisha miaka hiyo 100, hasa baada ya kuondokewa na mpendwa mke wake. Endelea na upendo huo huo na kusaidiana katika kila hali. Mbarikiwe sana. Anna
ReplyDelete