FRANCIS DASTAN BENDERA
Ndugu Allan Dastan Bendera mwana Diaspora wa Italy na mjumbe wa Jumuiya ya Watanzania Italy anasikitika kutangaza kifo cha mdogo wake pichani Francis Dastan Bendera, kilichotokea jana tarehe 6/01/2014 katika hospitali ya Muhimbili Dar Es Salaam Tanzania.

Marehemu alikuwa amelazwa katika hospitali ya Muhimbili baada ya kupata ajali ya bus la BURUDANI lililokuwa likitokea Korogwe kwenda Dar Es Salaam .

Ajali hiyo ilitokea  Disemba 12 mwaka huu majira ya saa 1.30 asubuhi  katika Barabara Kuu ya Segera Chalinze  eneo la Kwaluguru Kata ya Kwedizinga  wilayani ya Handeni.

Mazishi yatafanyika kesho tarehe 08/01/2014 nyumbani kwao Korogwe.
Basi la Burudani alilopata nalo ajali marehemu Francis Dastan Bendera

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Mayange MgambaJanuary 08, 2014

    Mola ndio anaetoa na anaechukua. Kapumzike kwa amani marehemu Francis

    ReplyDelete
  2. aliyeferiki ni Allan Dastan Bendera Au Francis Dastan Bendera?

    ReplyDelete
  3. HAPANA ALIYEFARIKI NI FRANCIS BENDERA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...