Tarehe 6 Januari nikiwa nimepaki gari eneo la Benaco Salasala, Dar es Salaam mida ya saa 11:30 jioni niliingia kanisani kwenye maombi.

Muda mfupi baadae nilitoka nikakuta gari yangu imevunjwa lock ya mbele. Wezi waliiba bag jeusi lenye laptop na vitu vingine kama hard disc, lazer pointers na vitu vingine zikiwepo nyaraka muhimu. Miongoni mwa vitu vingine ni vyeti vya chuo kikuu cha Dar es Salaam na taarifa muhimu za tafiti mbalimbali.

Ninaomba kama kuna yeyote anayeweza kusaidia kupatikana au kwa vitu hivyo au baadhi awasiliane nami kwa SIMU namba 0687375296. zawadi nono itatolewa kwa atakayefanikisha upatikanaji wa vitu hivyo.

Computer ni aina ya PANASONIC ambazo hazipatikani hapa nchini kwa wingi, hata key za operating systems zake hazipatikani kwa vendors.

Nitashukuru sana kwa msaada au taarifa yoyote.
Wenu Mdau

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Kwanza,heri ya mwaka mpya wewe mdau uliyeibiwa.Pili,kesi kama yako zimesharipotiwa sana humu kwenye hii blog,ingawa hapa katikati zilipungua kidogo.Mimi narudia tena kusema-Uwe na gari la kisasa lenye vikorombwezo vya kila aina na central locking,tints za kimataifa.Kama una vitu vya thamani na nyaraka muhimu ndani ya gari,basi ukipark gari na kwenda sehemu ambayo hautaweza kulilinda au kuliona,teremka na vitu vyako vyote.Hii na pamoja na kwenye vyumba vya hotelini,migahawa,nk.We are not learning.Ni matumaini yangu vitapatikana,pole sana.

    David V

    ReplyDelete
  2. mm naona hayo maeneo uloibiwa tafuta kijiwe cha wavuta bangi tangaza dau utavipata

    ReplyDelete
  3. Hili swala la kuvicha vitu vya thamani ndani ya magari yetu tutaliongelea mpaka lini?....ok ndugu pole sana

    ReplyDelete
  4. Pole sana, ningekushauri rudi tena kwenye maombi wakupatie mwizi wako, ashindwe na alege kwa jina la Yesum

    ReplyDelete
  5. Si kila mtu anasoma habari iliyoandikwa humu, na kumbuka wasomaji wanaongezeka hivyo inawezekana kuwa mdau aliyeibiwa ni kati ya wasomaji wapya. Haiitaji misuli kufikiria hili . Ishu hapa ni kumsaidia mdau apate vitu vyake na kupambana na uhalifu wa namna hii.

    ReplyDelete
  6. Tafuta vijiwe vya wavuta bangi maeneo hayo tangaza dau. I believe utavipata.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...