Rais mpya wa Madagascar Hery Rajaonarimampianina akiapishwa rasmi rais wa nchi hiyo mjini Antananarivo kufuatia ushindi mkubwa alioupata katika uchaguzi mkuu uliofanyika nchini humo mwezi Desemba 2013.
Rais mpya wa Madagascar Hery Rajaonarimampianina akisani kiapo chake tayari kuanza kazi ya kuwatumikia wananchi wa Madagascar mbele ya Jaji Mkuu wan chi hiyo Jean –Michael Rasolonjatovo (kushoto) wakati wa sherehe za kumuapisha rais huyo zilizofanyika mjini Antananarivo.
Rais mpya wa Madagascar Hery Rajaonarimampianina akizungumza na wananchi wa Madagascar waliofurika ndani ya uwanja wa Antananarivo mara baada ya kuapishwa kuwa rais mpya wa nchi hiyo mjini. Picha na 5 na 6. Viongozi mbalimbali na wanachi waliohudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais mpya wa Madagascar Hery Rajaonarimampianina mjini Antananarivo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Bernard Membe akimuwakilisha Rais Jakaya Kikwete katika sherehe za kumuapisha rais mpya wa Madagascar akiwa kwenye jukwaa kuu pamoja na viongozi wengine wa nchi za Afrika waliohudhuria sherehe hizo mjini Antananarivo.Wengine wanaoonekana kutoka kulia ni Rais mstaafu wa Msumbiji Joachim Chisano, Rais wa Namibia  Ipikefunye Pohamba na aliyekuwa rais wa Madagascar Andry Raojolina.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Pohamba siyo rais wa Zambia!

    ReplyDelete
  2. waswahili wanasema kuwa na macho sio dalili za kuona sasa mdau hapo juu umeona wapi palipoandikwa pohamba rais wa Zambia?
    tafadhali tuonyeshe na sisi wenye makengeza.
    mdau.
    miwani,pemba.

    ReplyDelete
  3. Jina la mwisho la huyu rais mpya sidhani kama linaenea kwenye hati za kusafiria, ni refu sana.

    ReplyDelete
  4. Hongera Dk Kikwete na Mh. Membe kwa kuwasaidia watu wa Madagascar kumchagua Raid wao kwa amani. Wengi wetu tutayaona mengi mazuri yaliyofanywa na JK akishatoka madarakani

    ReplyDelete
  5. "...sidhani kama linaenea kwenye hati za kusafiria, ni refu sana."

    LINAENEA TU!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...