Mwenyekiti wa Baraza la Biashara la Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Said Meck Sadiq ambaye pia ni
Mkuu wa Mkoa huo (wa pili kulia) akisisitiza jambo wakati uzinduzi wa baraza hilo mwishoni mwa
wiki Dar es Salaam. kulia ni Kamishina wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Bw. Suleiman
Kova; Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC), Bw. Raymond Mbilinyi (kushoto) na
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bi. Theresia Mbando.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC), Bw. Raymond Mbilinyi (kushoto) akisisitiza
jambo wakati wa uzinduzi wa baraza la biashara la mkoa wa Dar es Salaam mwishini mwa wiki jijini
humo. Wengine ni Mwenyekiti wa baraza hilo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Said Meck
Sadiq (wa pili kulia), Kamishina wa Polisi, Kanda maalumu ya Dar es Salaam, Bw. Suleiman Kova
(kulia) na Katibu Tawala, Mkoa wa Dar es Salaam, Bi. Theresia Mmbando (wa pili kushoto).
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Wajumbe wa Baraza la Biashara Mkoa wa Dar es Salaam wamehimizwa kuunganisha nguvu zao pamoja ili baraza hilo liwe na nguvu kubwa ya kutekeleza majukumu yake kwa ajili ya kukuza biashara na uchumi wa mkoa na nchi kwa ujumla.
Mwenyekiti wa baraza hilo Said Meck Sadiq ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa huo aliwambia waandishi wa habari wakati wa kikao cha uzinduzi wa baraza hilo kuwa nguvu ya pamoja itasaidia mkoa kufikia malengo yake zaidi ya biashara na uchumi.
“Ili baraza liweze kuwa na nguvu na maamuzi sahihi wajumbe wote wanahitaji kushiriki kwa uzito wao,” alisema na kuongeza kuwa kwa kufanya hivyo watasaidia mkoa wao kuzidi kupiga hatua kibiashara.
Alisema uchumi wa nchi unategemea ushiriki wa sekta ya umma na sekta ya binafsi na baraza hilo liliundwa ili kuwa chombo kinacho wakutanisha kwa ajili ya maswala hayo.
Alisema pamoja na kwamba baraza la mkoa tangu kuzinduliwa mwaka 2007 halikuweza kufanya mikutano, kwa sasa litakuwa linakutana kila baada ya miezi mitatu kutokana na umuhimu wake.
Alifafanua kwamba baraza hilo ni semu muhimu kwa wafanyabiashara wa mkoa wake kuzungumza kero zote za kibiashara ili wote kwa pamoja waweze kuja na majibu ya uboreshaji shughuli za biashara.
“Hakuna sememu nyingine muhimu kwa sekta binafsi kusemea maswala yao kama hii,” alisema na kufafanua kuwa maswala kama ya msongamano wa magari na changamoto za mashine za risiti zinaweza kutatuliwa na baraza hilo.
Pia aliyasisitiza mabaraza ya wilaya zote tatu za Ilala, Temeke na Kinondoni kufanya mikutano haraka ili ajenda zao zifikishwe kwenye baraza la mkoa na kujadiliwa kwa maamuzi zaidi.
Naye Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC), Bw. Raymond Mbilinyi alisema kikao hicho kilikuwa cha maandalizi ya mkutano wa baraza unaotarajia kufanyika mwezi ujao baada ya baraza la mkoa kupata wajumbe wake wapya mwezi Novemba mwaka jana.
“Mabaraza kama haya yameonyesha mafanikio makubwa sana katika mikoa mingine hapa nchini,” alisema.
Alisema baraza la mkoa wa Dar es Salaam ni muhimu sana kwa vile thamani ya biashara inayofanyika katika mkoa huo inachangia kwa kiwango kikubwa uchumi wa Tanzania.
“Kikao hiki tumekifanya ili wajumbe waweze kufahamishwa kuhusu majukumu yao na tutaendelea kufanya hivyo ili kuwasaidia kutimiza majukumu ya baraza,” alisema.
Alisistiza kuwa sekta binafsi ni wabia wa maendeleo na kuwa TNBC itahakikisha inafanya kazi kwa karibu na baraza hilo ili kufikia malengo ya kibiashara yanayokusudiwa.
Baraza hilo la mkoa linaundwa na wajumbe 40, nusu kutoka sekta ya umma na wengine kutoka sekta binafsi.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...