Barabara mpya ya mkato inayokatiza Jangwani na kutokea Kigogo jijini Dar es salaam ambayo ina miaka kadhaa haijaisha na kuzua maswali yasiyo jibu hadi leo. Barabara hii inayojengwa kupunguza msongamano katika barabara za Morogoro road na Uhuru road hadi sasa imekamilika nusu tu, sehemu za Jangwani. 
Baada ya kufuatilia swala hili Globu ya Jamii imepata taarifa za uhakika kwamba kuna baadhi ya wamilliki wa majengo yanayotakiwa kupisha ujenzi huo wamegoma kuomndoka na wamefungua kesi mahakamani na hivyo kusababisha ujenzi huo kutoweza kuendelea katika maeneo husika. 
Hii ndiyo shida ya hapo ambayo hatma yake inasubiri  maamuzi ya mahakama kufuatia kesi hiyo iliyofunguliwa na watu 7 miaka mitatu iliyopita. Na hakuna kitachoendelea hadi hapo...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. bongo maisha bado magumu sana..ankal njoo uishi mamtoni angalau usogeze mbele umri wako wa kufa ankal..angalia hapo vumbi, nyumba zimejengwa ovyo ovyo, magari&bodaboda zinapishana bila kufuata sheria, hakuna njia za watembea kwa miguu, etc..ni shiiiida sana!

    mdau UK

    ReplyDelete
  2. Ni kweli naungana moja kwa moja na mdau wa kwanza....wajua kabla hata sijasoma ulichoandika, nilikua najisemea mwenyewe hayooo uliyoyatoa kama maoni hasa baada ya kuangalia hii video.....duh itabidi nivute vute kidogo.....yaani kero tupu..alafu hatari kila kona.....mengi yanachangai watu kuondoka ktk umri mdogo sana...yaani ubongo wangu ulichoka kwa kuangalia matukio yoote yaliyojiri ktk hii video...sasa pata picha ...kama ndio upo pale live ktk kindibwindwibi hiki unachoka haraka sana...

    ReplyDelete
  3. Ndio mawazo ya diaspora, kutafuta solution mjenge kwenu hamtaki mnafikiria kuwahamisha watu..hahaha...mzee michuzi komaa hapahapa mpaka kieleweke...

    ReplyDelete
  4. mdau anayesema bongo maisha shida ankal aje kuishi mamtoni na wewe utabaki hivyohivyo na ujinga wako bongo ni kwenu sio uk na utabaki kuwa kibaraka tu

    ReplyDelete
  5. it's very interesting to see negative view points of some Tanzanians in the diaspora about their homeland
    East or West Home is best.We kenyans always think of ways to develop our motherland. I have worked in Europe,US and Asia as an investment analyst and all indications are that Africa is the next frontier of investment

    ReplyDelete
  6. Kukimbia sio suluhisho, kumbuka kuwa ndugu zako kibao wapo wanakula hilo hilo vumbi. Cha muhimu ni kurudi na kubadilisha hayo mabaya, ukiweza kufanya hivyo basi hata ukifa una miaka 20 bado utakumbukwa kwa muda mrefu, na pia utakuwa ukiwa una cha kujivunia. Kuishi umri mrefu hakuna maana kama hautaweza kutumia muda wako duniani kubadilisha kibaya kuwa kizuri.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...