Mkuu wa mkoa wa Mwanza,Mh. Evarist Ndikilo (aliesimama) akitoa ripoti fupi mbele ya wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Wizara ya Nishati na Madini juu ya miradi inayotekelezwa na Wakala wa Umeme Vijijini walipomtembelea ofisini kwake ili kuelezea nia yao ya kufanya ziara katika mkoa huo.

Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Wizara ya Nishati na Madini wameanza ziara ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na wizara hiyo kupitia Wakala wa Umeme Vijijini (REA) katika mikoa ya kanda ya ziwa.

Wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Victor Mwambalaswa, kamati hiyo ilipata nafasi ya kupokea taarifa fupi kuhusu utekelezwaji wa miradi hiyo iliyosomwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo ambaye aliwaeleza namna sekta hiyo inavyochangia katika kuinua vipato vya wananchi na taifa kwa ujumla.

Akitoa taarifa kuhusu mahitaji ya umeme Mkoani humo alieleza kuwa kiasi cha juu kinachotumiwa na mkoa huo ni megawati 46 na kuongeza kuwa , kiasi hicho kinaonesha mahitaji halisi na umuhimu wa nishati hiyo na namna umeme unavyochangia ukuaji wa uchumi mkoani humo.

Akizungumza kuhusu ujenzi wa miundombinu ya umeme, alieleza kuwa ujenzi huo umeshika kasi na kuongeza kuwa tayari tayari mradi uliotekelezwa na Millenium Challenge Corporation (MCC) umekamilika wakati miradi mingine inayotekelezwa na REA na Electricity Five inaendelea ambapo takribani wilaya 9 za mkoa wa mwanza zimeguswa na miradi hiyo.

Aidha alisema mradi wa REA phase 1 unajegwa na mkandarasi toka Symbion umegusa wilaya ya Sengerema, Magu na Ukerewe, REA awamu ya pili utaigusa wilaya za Magu, Misugwi, Ukerewe, Sengerema na kwimba na kumalizia kwa mradi wa electricity five unaofadhiliwa na Benki ya Maendeleo Afrika kuwa unagusa wilaya za Magu, Misubwi, Kwimba, na Sengerema ambapo alisema katika mradi huo ulipwaji wa fidia kwa wananchi watakaoathirika umeshaanza.

‘‘Kazi ya usambazaji wa umeme Mkoani Mwanza inakwenda vizuri, kukamilika kwa miradi hii kutasaidia vijiji vingi kuwasha umeme hivyo kukuza pato la taifa’’ alisema Ndikilo.

Alimalizia kwa kuwataka wajumbe hao kuwafahamisha wananchi kutumia vipato na akiba zao katika kujenga nyumba zenye ubora ili waweze kuunganishwa na huduma ya umeme.

Vilevile Mhe Ndikilo aliwaomba wajumbe kuwaeleza wananchi wanaowahudumia kujenga mazoea ya kuwa na mwamko wa kupokea na kupenda maendeleo yanayopelekwa kwao na serikali.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati jhiyo Mhe. Victor Mwambalaswa akipokea taarifa hiyo alieleza kuwa nia ya serikali ni kuhakikisha kuwa idadi ya watu waliounganishiwa umeme inapanda toka asilimia 14 hadi kufikia asilimia 30 ifikapo 2015.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...