
Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi ya Diamond juu ya umuhimu wa kujifunza mauaji ya kimbari ya wayahudi ya mwaka 1933.
Na Mwandishi Wetu
Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) kimeendelea kutoa mafunzo na elimu juu ya umuhimu wa kukumbuka maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya ukombozi wa kambi za mateso ya Auschwitz kwa wanafunzi wa sekondari na shule za msingi nchini.
Akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi ya Diamond ya jijini Dar es Salaam leo asubuhi, Afisa habari wa kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama amesema kwamba ni muhimu kwa kizazi na kizazi kujifunza madhara ya mauaji na maangamizi ya moto dhidi ya wayahudi yaliofanywa na askari wa kinazi wa Ujerumani.
“Ni muhimu kutoa mafunzo kwa vijana wakitanzania wa shule za msingi na sekondari ili wajue kwamba tofauti za rangi na za kidini hazina nafasi ya kutugawa kama binadamu,” amesema Nkhoma.
Sasa kumbukumbu ya mateso ya waisrael ni ya nini kwenye shule zetu? Kwa nini tusiwakumbuke mababu zetu waliouawa na haohao wajarumani kwenye vita ya majimaji?
ReplyDeleteBetter teach them about slave trade sip wayahudi
ReplyDeleteNa mateso ya wapalestina yatasomeshwa pia?
ReplyDelete