JUMUIYA ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) imeunga mkono kazi zinazofanywa na sekretarieti ya chama cha Mapinduzi chini ya Katibu Mkuu Abdulrahaman Kinana huku ikiwatupia lawama baadhi ya vigogo kutokana na kukwamisha juhudi hizo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam Katibu wa Uhamasishaji na Chipukizi, Paul Makonda amesema, vijana wa UVCCM wanatambua na kuthamini juhudi za Katibu Mkuu na Sekretarieti yake katika kukijenga chama kwa kusimamia barabara misingi na shabaha ya kuundwa kwake.

Makunda alisema, inapofika wakati wasimamizi wa chama wanapoanza kupigwa  vita juu ya kusimamia kanuni za chama hii siyo sahihi.

“Haiwezekani matajiri na watu wenye uchu wa madaraka watake kukihodhi na waratibu mikakati ya kukihujumu kwa pesa zao hali sisi vijana tukitazama, tunasema kutakilinda chama chetu na tutawalinda viongozi wetu waadilifu”Alisema.

Hata hivyo Makunda alisema, wanaobezwa leo  kuwa wanaharibu chama ndiyo wameweza kurudisha imani ya wananchi kwa chama , imani na matumaini ambayo tayari yalishaanza kupotea na chama kuonekana si tena cha wanyonge, wakulima na wafanyakazi wa nchi hii.

Aidha Makunda alisema, mtu anayebeza ziara zilizofanyika na kuwaita viongozi walizozifanya ziara hizo ni waropokaji na wahuni anapaswa kuchukuliwa hatua kali za kinidhamu ili iwe fundisho kwa wengine.

“Muhuni ni mtu mjinga, mtu wa hovyo, hana maadili, asiyependa chama, mhaini na mzandiki anayepaswa kuchukuliwa hatua kali za kinidhamu ili iwe fundisho kwa wengine” Alisema Makonda.
 Katibu wa Uhamasishaji na Chipukizi, Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
 Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika mkutano huo.
  Katibu wa Uhamasishaji na Chipukizi, Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, wakati akitoa tamko la Jumuiya ya Vijana wa CCM kuunga mkono kazi ya sekretarieti ya Chama cha Mapinduzi chini ya Katibu Mkuu, Mh. Abdulrahaman Kinana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. HONGERA SANA PAUL MAKONDA KWA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA MH.KINANA,KWA MUDA MFUPI TOKA ATEULIWE KUSHIKA WADHIFA WA KATIBU MKUU AMERUDISHA IMANI YA WAPIGA KURA KWA CCM.NAOMBA PIA MUMKEMEE GUNINITA KWA KUMBEZA NAPE.GUNINITA ANA AJENDA YAKE,EITHER NI NJAA,ANATUMIKA KUCHAFUA WATU.ALIISHAWAHI KUWA MPINZANI,HANA SERA,MKEMEENI KWA NGUVU ZOTE.

    ReplyDelete
  2. Huyu dogo hajui nini maana ya leadership....

    Uteuzi wa mawaziri ndiyo ulioonyesha kuwa Kinana na Nape wanakivuruga chama wala siyo watu wengine labda kama Makonda ataniambia hao watu wenye hela wamemnunua Rais hapo ntakubali.

    Dogo nenda darasani kajifunze maana ya leadership......Where is responsibility of choice and authenticity kwa Kinana na Nape, na chama kwa ujumla kama mawaziri mizigo mpaka leo bado wapo madarakani....

    Why did they tell us kuwa mawaziri ni mizigo....then bado tunawaona?

    We dogo wewe!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...