Mume wa marehemu Dullah na mdogo wa marehemu Ngalu Buzohera wakiwa kwenye harambee ya kuchangisha fedha za kusaidia kusafirisha mwili wa mpendwa wetu marehemu Zainab Buzohera aliyefariki Jumamosi Jan 4, 2014 saa 2 usiku (8pm ET) WanaDMV walijumuika katika harambee iliyofanyika Bladensburg, Maryland na kuchangisha $22,938 kiasi kilichokuwa kinatakiwa ni $15,000 hii inamaanisha wanaDMV wanapoamua hufanya kweli shukurani kwa wote walioshiriki harambee hii kwa njia moja au nyingine lengo ni kufanikisha na Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema tunashukuru kwa kutuwezesha kufanikiwa harambee hii ya mpendwa wetu Zainab Buzohera. WanaDMV tunawashukuru wenzetu wa New York waliofika kwenye harambee hii kuja kusaidia kutimiza malengo.
Shangazi wa marehemu Jasmine Bernett akiongea kwa niaba ya familia ya Buzohera huku akiwa amejawa na uso wa huzuni aliwashukuru  wote waliofika kwani lengo ni kusaidia kuchangia ili mwili wa marehemu Zainab uweze kusafirishwa nyumbani Tanzania kwa mazishi na matarajio ni kusafirisha siku ya Jumatano na kisomo kinatarajiwa kufanyika siku ya Jumanne jioni mahali patatangazwa baadae.
Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV Bwn Idd Sandaly akielezea utaratibu wa harambee.
Umati wa Watanzania waliokuja kwenye harambee.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hey! So Sad jamani, what went wrong? I know this Dada and part of their family, Tunaomba ratiba nzima ili tuwepo na sie huku bongo. Poleni sana wakina Buzohera, Ngalu Pole Mama.

    Ndimi
    - D -

    ReplyDelete
  2. Inna lillahi waina illahi rajiun. Vifo kama hivi vinatia huzuni maana sio vya kutokea kwenye taifa kubwa!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...