Na Faustine Ruta, Bukoba
TIMU ya Mbeya City leo imeanza mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Vodacom vyema baada ya kuifunga Kagera Sugar kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Kaitaba mjini Bukoba kwa bao 1-0 leo.
Kipindi cha kwanza kilimalizika kikiwa hakuna timu iliyokuwa imeziona nyavu za mwenzake hivyo zikalazimika kwenda mapumziko zikiwa 0-0
Kipa wa Kagera Sugar Hannington akiwa hoi kwa kuumia mguu baada ya kuachia frii kiki na kushtua mguu na kulazimika kutolewa nje katika kipindi hicho cha kwanza.
Kipindi cha pili katika dakika ya 72 Mbeya City walipata bao kupitia mchezaji wao Richard Peter aliyekuwa amevaa jezi no. 13 mgongoni. Hadi tunaenda mitamboni mji wa Bukoba na vitongoji vyake ulikuwa kimya kama kuna msiba vile, wakati maripota wetu huko Mbeya wanasema mji wote ulizizima kwa furaha na nderemo....
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...