Mkurugenzi
wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media Group,Ruge Mutahaba akitoa
maelezo mafupi kwa Waziri Mkuu Mstaafu,Mh.Frederick Sumaye kuhusiana na
urushaji wa matangazo kwa njia ya kisasa ndani ya studio kuu ya redio
Clouds FM,Sumaye amefanya ziara fupi mjengoni humo na kujionea shughuli
mbalimbali zinazofanywa na kampuni hiyo zikiwemo na urushaji wa
matangazo ya redio na Televisheni kwa ujumla.
Mmoja
wa Watangazaji kipindii cha Michezo Clouds FM,kiitwacho Sports Extra,
Ibrahim Masoud a.k.a Maestro akifanya mahojiano mafupi na Waziri Mkuu
Mstaafu,Mh.Frederick Sumaye kuhusiana ushabiki wake mkubwa kwa timu ya
Simba sambamba na migogoro iliyoikumba club hiyo ya Msimbazi
Ruge
Mutahaba akitoa ufafanu mfupi kwa Waziri Mkuu Mstaafu,Mh.Frederick
Sumaye,kuhusiana na Kifaa maalum na cha kisasa cha kurushia matangazo ya
biashara,pichani nyuma ni Mkuu wa Kitengo cha Habari Clouds FM,Joyce
Shebe akisikiliza.
Waziri
Mkuu Mstaafu,Mh.Frederick Sumaye akiwa kwenye chumba cha kurekodia
mahojiano mbalimbali,akiwa amekutana na wadau wa Mfuko wa Dhamana ya
Uwekezaji Tanzania (UTT),pichani kulia ni Afisa Masoko Mwandamizi wa
UTT,Mfaume Kimario na Afisa Masoko na Uhusiano,Bwa.Rahim Mwanga.
Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media Group,Ruge Mutahaba akitoa maelezo mafupi kwa Waziri Mkuu Mstaafu,Mh.Frederick Sumaye kwenye moja ya Ofisi za kampuni hiyo,alipofanya ziara fupi mjengoni humo na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na kampuni hiyo zikiwemo na urushaji wa matangazo ya redio na Televisheni kwa ujumla. pichani kati anaeshuhudia ni Ofisa Mahusiano wa Clouds Media Group,Simon Simalenga.
Mkuu wa Kitengo cha Habari Clouds FM,Joyce Shebe akitoa ufafanuzi mfupi kwa Waziri Mkuu Mstaafu,Mh.Frederick Sumaye alipotembelea kitengo hicho cha habari na kujionea uandaaji wa habari ya televisheni na redio unavyofanyika.
Ruge Mutahaba akimtambulisha Mkurugenzi mwanzake wa Maendeleo ya Biashara,Sheba Kussaga kwa Waziri Mkuu Mstaafu,Mh.Frederick Sumaye.
PICHA ZAIDI BOFYA MICHUZIJR.BLOGSPOT.COM
PICHA ZAIDI BOFYA MICHUZIJR.BLOGSPOT.COM
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...