Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Rashid Seif Suleiman akimkaribisha Waziri Mkuu wa Finland Jyrki Katainen alipkutana na uongozi wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) Kempasi ya Vuga alipofanya ziara ya siku moja Zanzibar.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) Professa Idrss Ahmad Raia akiteta jambo na Waziri Mkuu wa Finland Jyrki Katainen alipotembelea chuo hicho Kempasi ya Vuga alipokuwa na ziara ya siku Zanzibar.
Waziri mkuu wa Finland Jyrki Katainen akizungumza na uongozi wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) alipotembelea chuo hicho katika ziara yake ya siku moja Zanzibar (wa kwanza kulia) ni Waziri wa Miundombinu na Mwasiliano Rashid Seif Suleiman na (kati kati) ni Makamu Mkuu wa Chuo hicho Professa Idriss Ahmad Rai.
Baadhi ya wahadhiri na viongozi wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar wakimsikiliza Waziri Mkuu wa Finland Jyrki Katainen wakati akiwahutubia katika Kempasi ya Vuga wakati wa ziara yake ya siku moja Zanzibar.
Picha ya pamoja ya Waziri Mkuu wa Finland na baadhi ya wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar na viongozi aliofutana nao kutoka Tanzania Bara. (wa kwanza kushoto) ni Balozi wa Finland nchini Tanzania Sinikka Antila.(Picha na Makame Mshenga wa Maelezo Zanzibar).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hongera Wahadhiri wa SUZA. "SKY IS LIMIT".

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...