Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe(kushoto), akimtabulisha Katibu
Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Shaaban Mwinjaka(aliyevaa tai nyekundu) kwa Waziri
Mkuu wa Finland, Jyki Katainen, wakati Waziri Mkuu huyo alipotembelea Mamlaka ya
Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA), leo asubuhi kuangalia shughuli mbalimbali
zinazofanywa na Mamlaka hiyo.
Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Awadh Massawe akitoa ufafanuzi wa
namna Bandari ya Dar es Salaam inavyofanya kazi kwa Waziri Mkuu wa Finland, Jyki
Katainen(wa tatu kutoka kushoto) , wakati alipotembelea Mamlaka hiyo leo asubuhi kuangalia
shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mamlaka. Kulia kwa Waziri Mkuu wa Finland ni Waziri
wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe na kushoto kwa Waziri Mkuu huyo ni Waziri wa
Niashati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania
(TPA), Mhandisi Madeni Kipande, akitoa maelezo ya awali ya namna ambavyo Bandari ya Dar
es Salaam inavyofanya kazi kwa Waziri Mkuu wa Finland, Jyki Katainen wakati alipotembelea
Mamlaka hiyo leo asubuhi kuangalia namna Mamlaka hiyo inavyofanya kazi. Aidha, Waziri
Mkuu huyo alitembelea Gati namba 1-7.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Shaaban Mwinjaka akichangia mada
wakati wa Mkutano na Waziri Mkuu wa Finland, Jyki Katainen alipotembelea Mamlaka ya
Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) leo asubuhi kuangalia utendaji wa Mamlaka hiyo.
Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe akimkabidhi zawadi Waziri
Mkuu wa Finland, Jyki Katainen wakati alipotembelea Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari
Tanzania(TPA), kuangalia utendaji wa Mamlaka hiyo. Nyuma ya Waziri Mwakyembe ni Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA).Picha na kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Uchukuzi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...