Waziri wa Fedha Mh. Saada Mkuya Salum akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) leo jijini Dar es salaam kushoto ni Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) Rished Bade.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano wa Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum katika ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO) Leo Jijini Dar es Salaam.
--
Na Frank Mvungi
Serikali imesema pato la Taifa limeendelea kukua kwa asiliamia 7 kwa mwaka katika kipindi cha mwaka 2012 hadi 2013 kutokana na mikakati mizuri ya maendeleo iliyotekelezwa kwa kuzingatia dira ya Taifa ya maendeleo.Hayo yamesemwa na Waziri wa fedha Mh.Saada Mkuya Salum wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.
 
Saada alibainisha kuwa katika robo ya tatu ya mwaka 2013 kiwango halisi cha ukuaji wa uchumi kilikuwa asilimia 6.5 ikilinganishwa na asilimia 7.2 katika kipindi kama hicho cha mwaka 2012.
 
Katika hatua nyingine Saada alisema kuwa Serikali imejipanga kuongeza pato kwa ufanisi zaidi ili kuongeza pato la Taifa na kupunguza ukwepaji wa kodi kwa kuboresha mifumo ya ukusanyaji kodi na kuwa ya kisasa zaidi.Aliongeza kuwa Serikali kupitia mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) itaendelea kutoa elimu ya matumizi ya mashine za kielektroniki ili kusaidia wananchi kuelewa umuhimu wake kwa maendeleo ya Taifa.
 
Hata hivyo alibainisha kuwa Serikali imekubaliana na wafanyabiashara kuwa mwisho wa kuanza kutumia mashine za kielektroniki umesogezwa hadi tarehe 30 januari, 2014 ili kuwapa wananchi muda wa kujiandaa na kuanza matumizi ya mashine hizo.
 
Pia alitoa rai kwa wadau wote kutoa ushirikiano wa dhati katika utekelezaji wa azma ya kuboresha mapato ya Serikali ili kuwaletea wananchi maendeleo endeleo.
 

Wizara ya Fedha imekuwa ikitimiza majukumu  yake kwa kuzingatia Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025,Mkakati wa kukuza uchumi na kupunguza umasikini (MKUKUTA) malengo ya maendeleo ya Milenia (MDGs) Ilani ya Uchaguzi mkuu ya CCM  ya mwaka 2010.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...