Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akiwa pamoja na Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Marcel Escure (kulia kwa Waziri) pamoja na Waziri Mstaafu wa Viwanda na Nishati wa Ufaransa Bw. Eric Besson (kulia kwa Balozi), pamoja na watendaji kutoka Ubalozi wa Ufaransa na Wizara ya Nishati na Madini, wakati walipomtembelea wizarani ili kufahamu fursa za uwekezaji katika sekta hizo.
Waziri wa Nishati na Madini , Profesa Sospeter Muhongo (wa kwanza kulia) , Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Marcel Escure (kulia kwa Waziri), Waziri mstaafu wa Viwanda na Nishati kutoka nchini Ufaransa Bw. Eric Besson (kulia kwa Balozi), pamoja na mtendaji kutoka Ubalozi wa Ufaransa nchini, wakifurahia jambo mara baada ya kumaliza mazungumzo yaliyolenga katika kuendeleza sekta za Nishati na Madini nchini.
Na Teresia Mhagama
Balozi wa Ufaransa nchini Bw. Marcel Escure akiongozana na
Waziri mstaafu wa Viwanda na Nishati kutoka nchini Ufaransa,
Bw. Erick Besson wamemtembelea wizarani Waziri wa Nishati
na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ili kufahamu fursa za
uwekezaji katika sekta za Nishati na Madini.
Waziri huyo mstaafu wa Ufaransa, Bw.Erick Besson alikuwa
akiiwakilisha kampuni ya GDF Suez ya Ufaransa.
Katika suala la usimamizi wa bomba la gesi asilia, Profesa
Muhongo alimweleza Bw. Besson kuwa Shirika la Maendeleo
ya Petroli (TPDC) litahitaji kupata uzoefu na pengine mbia
aliyebobea katika usimamizi wa bomba hilo atakayeshirikiana na
TPDC katika usimamizi wa bomba la gesi nchini.
Kuhusu umeme, Waziri Muhongo alimweleza Waziri mstaafu
huyo wa Ufaransa kwamba serikali inajikita katika miradi ya
usambazaji umeme kwa utaratibu wa ubia au mikopo ya bei nafuu
na ina mpango wa kujenga njia ya umeme ya msongo wa 400kv
kuelekea ziwa Tanganyika hivyo aliikaribisha kampuni ya GDF
Suez kuwekeza katika miradi hiyo ya usambazaji umeme.
Aidha Profesa Muhongo alimweleza Bw. Besson kuwa Shirika la
Madini la Taifa (STAMICO) linatafuta mbia watakayeshirikiana
naye katika kuendesha mtambo wa kuzalisha umeme kwa
kutumia makaa ya mawe, Kiwira mkoani Mbeya hivyo kama wana
nia ya kuwekeza katika eneo hilo pia wanakaribishwa kuingia
katika ushindani wa kupata nafasi hiyo.
Naye Waziri mstaafu wa Viwanda na Nishati kutoka nchini
Ufaransa, Bw. Besson alimshukuru Profesa Muhongo kwa taarifa
nzuri kuhusu fursa za uwekezaji nchini na ameahidi kupata taarifa
zaidi za uwekezaji katika mashirika ya TPDC, STAMICO na
TANESCO ili kuona jinsi kampuni ya Suez itakavyoshirikiana na
mashirika hayo katika kuendeleza sekta za Nishati na Madini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...