Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhe. Mathias Chikawe (katikati) akiwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. Pereira Silima na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini,IGP Ernest Mangu pamoja na maofisa wakuu wa Jeshi la Polisi wakiimba wimbo wa Maadili wa Jeshi la Polisi wakati Waziri Chikawe alipofanya ziara katika idara ya Polisi Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Dar es Salaam leo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe akipokea hati ya maboresho ya Jeshi la Polisi, mpango kazi wa Jeshi la Polisi Pamoja na kitabu chenye miongozo ya Jeshi la Polisi kutoka kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Ernest Mangu Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam leo,alipoanza kufanya ziara katika idara za Wizara aliyokabidhiwa kuiongoza hivi karibuni.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mathias Chikawe (aliesimama), akizungumza na maofisa wakuu waandamizi wa Jeshi la Polisi nchini, Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam alipoanza kufanya ziara katika idara za Wizara aliyokabidhiwa kuiongoza hivi karibuni. Kulia ni Naibu Waziri Mambo ya Ndani Mhe. Pereira Silima na kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Ernest Mangu. Picha Na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...