
Jumla ya vikundi 32 kutoka ndani na nje ya nchi vimechaguliwa kufanya maonyesho ya muziki katika tamasha la 11 la Sauti za Busara ambalo limepangwa kufanyika kuanzia tarehe 13 mpaka 16 Februari 2014 katika viwanja vya kihistoria Ngome Kongwe, zanzibar.
Orodha ya wasanii imejumuisha imejumuisha wasanii maarufu kutoka Africa Mashariki, Kusini na Afrika Magharibi, pamoja na wasanii kutoka nchi za Mto Nile na hata maeneo ya Puerto Rico
Sauti za Busara (Sound of Wisdom) linalojulikana kama ‘Tamasha rafiki katika Sayari’ ni tamasha la kimataifa linalosheherekea muziki wa kiafrika kila mwaka wiki ya pili ya mwezi wa Februari. Lengo likiwa ni kuwaleta watu pamoja na kuonyesha utajiri wa muziki wa kisasa ambao umebuniwa katika nchi za Afrika Mashariki, nchi nyingine kutoka barani Afrika na kwingineko duniani.
Wasanii watakaopanda jukwaani kutoka hapa nyumbani ni pamoja na Jhikoman nguri wa muziki wa Rege anayesifika hapa nchini na ambae ameshafanya maonyesho mbalimbali ya muziki ndani na nje ya nchi, ambapo kwa upande wa Sauti za Busara hii ni mara yake ya nne kupanda jukwaani. Jhikoman mpaka hivi sasa amesha toa albam tatu zinazojulikana kama Chikondi aliyoitoa mwaka 2005, Tupendane, 2008 na Yapo, iliyoingia sokoni mwaka 2009.
kiingilio ni ngapi?
ReplyDelete