Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini,Mh. Zitto Z. Kabwe pamoja na Mwanasheria wake,Albert Msando (kulia) wakiwasili katika Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam leo huku wakiongozana na wafuasi wanaopinga kuvuliwa uongozi wake,tayari kwa kwenda kusikiliza kesi yake aliyoifungua dhidi ya Chama Chake cha CHADEMA inayosikilizwa leo Mahakama Kuu.
Mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini ameshinda kesi yake hiyo aliyoifungua akiitaka Kamati Kuu ya Chadema kutojadili Uanachama wake hadi kesi ya msingi aliyoifungua itakaposikilizwa.
Habari zaidi utaendelea kuzipata hapa
Wafuasi wa Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini,Mh. Zitto Kabwe wakimshangilia kiongozi wao alipokuwa akiwasili Mahakamani hapo leo.
Sehemu ya Wafuasi wa CHADEMA wasiomkubali Zitto Kabwe wakiwa na Mabango yao nje ya Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam leo.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
THIS IS A VERY SAD PICTURE. MUNGU IBARIKI TANZANIA. Kwa kutumia maagizo ya mwalimu wangu wa lugha wa darasa la sita, ichunguze picha hii kisha uandike insha.
ReplyDeletesasa hapa inshu ni kuwa CHADEMA hawataki kupeleka kesi ya ZZK kwenye Baraza Kuu ama? Maana huu mchezo wote wa redio unazidi kukiumiza chama. Mpelekeni tu Baraza Kuu msiogope kushindwa ndio demokrasia hio!!
ReplyDeleteHao wafuasi na mabango yao wanaisadia au kuibomoa CDM? Au wanaonyesha tu true face ya chama chao!
ReplyDeleteChadema ndembendembe..nyarinyari...chaliii pwaaaataaaa.
ReplyDeletehayo matusi ndio demokrasia ya chadema? kuanzia uongozi wa juu mpaka wafuasi wake wote hekima hawana, busara ya mtu inaonekana kwa mazungumzo, muonekano, hata hayo mabango mliyobeba yangewaonyesha hekima zenu. hebu kaeni chini mtafakari, mtasema ni zito mbaya kumbe nyie wenyewe ndio wabaya:
ReplyDelete1. yawezekana mna ubinafsi katika uongozi wenu, hamshirikishani katika maamuzi.
2.acheni uroho wa madaraka, la sivyo mwakani hampati kitu, bado siku tu uchaguzi. mnagombana wenyewe kwa wenyewe.
3. slaa waachie wengine sasa uone nao watafanya nini?
4. slaa nenda kwenu katengeneze chama kuanzia nyumbani kwako, maana kwako sidhani kama unakubalika, ukitengeneza kwako, kwingine itakuwa mteremko tu.
4. mbowe, uache kauli kali, watanzania hawakuzoea hayo, ndiyo maana mnaona watoto ndio wengi kwenye mikutano yenu, mwisho wa kupiga kura hakuna kitu. rekebisheni kauli. waswahili husema kauli ni mali.
5. ikiwa mtajirekebisha kwa hayo, hata mimi nitawapigia kura.
michuzi usinibanie.