Na. Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma.

Askari polisi watano mkoani dodoma wafariki dunia papohapo katika ajali ya gari iliyotokea 31/01/2014 majira ya 23.45 hrs katika barabara kuu ya Dodoma – Morogoro eneo la Mtumba Center, Kata ya Mtumba Tarafa ya Kikombo Manispaa ya Dodoma, ambapo gari namba T.770 ABT Toyota Corolla lililokuwa likiendeshwa na Askari namba H. 3783 PC DEOGRATIUS wa Polisi Wilaya ya Kongwa likitokea Dodoma mjini likielekea Wilayani Kongwa liligongana uso kwa uso na gari namba T.997AVW Scania Bus mali ya Kampuni ya Mohamed Trans lililokuwa likiendeshwa na JUMA s/o MOHAMED, miaka 38, Mkazi wa Mwanza, likitokea Dar es Salaam kuelekea Dodoma na kusababisha vifo kwa askari watano papohapo. 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME amewataja Askari hao waliofariki katika ajali hiyo kuwa ni:-
1.          D.9084 D/CPL. ADOLF S/O MESHACK SILLA mwenye miaka 51, Mgogo.
2.          F.6459 D/C. EVARIST s/o MOSES BUKOMBE mwenye miaka 34, Muha.
3.          H.3783 PC. DEOGRATIUS s/o PATRICK MAHINYILA mwenyw miaka 29, Mgogo.
4.          WP.10337 PC. JACKLINE d/o AUGUSTINE TESHA mwenye miaka 22, Mchaga.
5.          WP.10382 PC. JEMA d/o JIMMY LUVINGA mwenye miaka 20, Mhehe. 
Wote ni askari Polisi Wilaya ya Kongwa na hakuna abiria aliyeumia katika basi.

Kamanda MISIME amesema chanzo cha ajali hiyo kulingana na uchunguzi wa awali ni mwendo kasi kutokana na uharibifu uliotokea kwa gari dogo walilokuwa wamepanda askari na jinsi lilivyoburuzwa na basi kwa umbali wa mita 56 kisha kwenda kusimama umbali wa mita 97, kwa hali hiyo umbali kutoka eneo walipogongana hadi basi liliipoenda kusimama ni mita 152. Dereva wa Bus alitoroka mara baada ya ajali hiyo kutokea, juhudi za kumtafuta zinaendelea. Miili ya maerehemu imehifadhiwa chumba cha maiti Hospitali ya mkoa Dodoma.

Aidha Kamanda MISIME ametoawito kwa madereva kila mara wawe na udereva wa tahadhari na na kuzingatia sheria za usalama barabarani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Mungu awalaze marehemu mahala pema peponi hao askari,pole kwa familia.Nimeandika humu mahali,Vifo vya ajali Tanzania ni vingi sana.MWAKA WA 2014 uwe wa kupunguza/kuzuia AJALI TANZANIA.Na hili basi kwanini linatembea usiku?Maeneo hayo lilitakiwa liwe limepita kati ya saa 8-9 mchana.

    David V

    ReplyDelete
  2. Uzembe wetu unatumaliza, nahamini kabisa hizi ajali zingeepukika..

    Mungu awalaze pema waliotutoka.

    ReplyDelete
  3. RIP waliopatwa na mauti.

    Ila huyo polisi kwanini anawatambulisha hao polisi kwa kabira?? Haina maana

    ReplyDelete
  4. This is very very sad kwa kweli. Jamani mpango wa upanuaji wa barabara kuwa wa two lanes ungepewa kipaumbele kwa barabara busy kama hizi. Watu wanaokufa kwa ajali ni sawasawa na wale wanaokufa katika mafarakano ya vita vya wenyewe kwa wenyewe central afrika. Tulione jambo hili kama ukosefu wa amani vile labda ndipo tutalishughulikia.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...