Mabomu ya machozi yametumika kuwatawanya wakulima wa eneo la Melela, Mvomero mkoani Morogoro waliokuwa wamefunga barabara ya Iringa - Morogoro wakimtaka Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera aende kusuluhisha mgogoro uliopo baina yao na wafugaji.
Wakulima hao ambao wanalima katika Mashamba yaliopo eneo la Mkangazi,Wilayani Mvomero,walilazimika kufunga barabara hiyo ili iwe shinikizo la kufika kwa Mkuu huyo wa Mkoa na kuwasikiliza ikiwezekana kutatua kabisa tatizo lao.
Wakulima hao wanadai kuwa wenzao watano jana wamevamiwa na wafugaji wa kabila la Wamasai na kujeruhiwa vibaya kwa vitu vyenye ncha kali na kupelekea kulazwa katika Hospitali ya Mkoa Morogoro.
Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Anthony Mtaka alifika katika eneo hilo mapema leo na kutaka kuwasikiliza wananchi hao,ambao wakati huo walikuwa wamechoma matairi kukata miti,hali iliyopelekea kuwepo kwa mgongamano mkubwa wa magari yaendayo mikoani,lakini wakulima hao walikataa kumsikiliza na kumtaka aje Mkuu wa Mkoa.
Baada ya vurugu kuwa kubwa, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile aliwaaamuru vijana wake wakatulize ghasia hizo na kuwataka wakulima kuondoka katika eneo hilo na wale waliokaidi walikamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi.Kwa sasa hali kidogo imetulia na magari yameanza kupita eneo hilo.
Askari wa Jeshi la Polisi Wakiwa Onyo wakulima wa Kijiji Hicho Kabla ya Kuanza Kutumia Mabomu ya Kutoa Machozi kwa Lengo la Kuwatanya.
Askari wa Polisi wa Kikosi cha kutuliza Ghasia akizima Moto uliowashwa na wakulima waliofunga barabara ya Morogoro Iringa mapema leo Asubuhi.
Wananchi wa Kijiji cha Mangae wakiwa wamefunga Barabara wakiwa wameshika mawe na Silaha za Jadi wakikataa kabisa kufungua barabara hiyo wamkitaka Mkuu wa Mkoa kuja Kuoanana Nao.Picha na Matukio TZ
Haya mabo ya kujichukulia sheria mkononi yakemewe kabisa. Kama kuna kero viongozi watengeneze mabaraza na vikao vya kusikiliza au kutatua shida zilizopo. Tusifikie hatua ya kuleta fujo.
ReplyDelete