Balozi wa Kudumu wa Ubalozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa,Geneva,Mhe. Balozi Modest J.Mero amekutana na Dr. Margert Chan, Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani, katika ofisi za Shirika la Afya Dunia jana tarehe 31 Januari 2014.
Huu mkutano ni moja ya mikutano ambayo Mhe Balozi anafanya na wakuu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa yenye makao makuu hapa Gevena, Uswisi Katika kajenga mahisiano ya karibu kikazi.
Katika mkukutano huu msimamo wa Tanzania kuhusu masuala mbalimbali ya Afya yalijadiliwa.
Maeneo ya kipaumbele ya ushirikiano na shirika hili ni pamoja na kutimiza maelengo ya millenia (MDGs), kuuipa kipaumbele maendelo na ustawi wa jamii na kuhakikisha Afya ina pewa kipaumbele baada ya mwaka 2015. Moja ya maeneo muhimu ya kuendeleza ushirikiano kati Tanzania na Shirika hili, ni eneo la kuboresha upatikanaji wa dawa na chanjo bora, kwa kuangalia jinsi Tanzania itakavyo weza kuwa na viwanda vyenye uwezo huo, na kupunguza utegemizi kutoka nje ya nchi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...