Makamu wa Pili wa Rais Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Balozi Idd Seif akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Malaysia Dkt. Aziz Ponary Mlima alipokwenda kumtembelea Ofisini kwake Zanzibar. Dkt. Mlima alikwenda kujitambulisha na kuwaaga viongozi wa Juu wa Kitaifa Zanzibar, na alikutana na Makamu wa Kwanza Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Seif Shariff Hamad.
Dkt. Mlima aliteuliwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete kwenda kuwa Balozi wa Tanzania nchini Malaysia na makazi yake yatakuwa Kuala Lumpur.
Ubalozi huo wa Tanzania nchini Malaysia pia una jukumu la kuiwakilisha Tanzania katika nchi zifuatazo: Malaysia, Indonesia, Philipines, Thailand, Cambodia, Laos na Brunei.
Makamu wa Pili wa Rais Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Balozi Idd Seif akiongea na Balozi wa Tanzania nchini Malaysia Dkt. Aziz Ponary Mlima alipokwenda kumtembelea Ofisini kwake Zanzibar.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...