Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli (aliyenyoosha mikono) akitoa taarifa kuhusu maendeleo ya utekelezaji wa ujenzi wa barabara za kupunguza msongamano katika jiji la Dar es Salaam wakati alipokutana na Kamati ya Bunge ya Miundombinu. Kulia kwa Waziri Magufuli ni Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi Eng. Gerson Lwenge na anayefuata ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Joseph Nyamhanga. Kushoto kwa Waziri ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Mhe. Peter Serukamba na wengine ni Wajumbe wa Kamati hiyo pamoja na Wataalam kutoka Wizara ya Ujenzi.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Mhe. Peter Serukamba (mbele mwenye koti la suti) akiwaongoza Wajumbe wa Kamati hiyo ya Bunge kukagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Segerea Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Ujenzi Mhe. Eng. Gerson Lwenge akitoa maelezo kwa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu kuhusu ujenzi wa barabara ya Mbezi kupitia Malambamawili kuelekea Kifuru hadi Kinyerezi.
Jiji la Dar limejengwa vibaya bila ya "Strategy" ndio maana sasa matatizo yanajionesha dhahiri. Hebu Waziri wa Mawasiliano na Ujenzi atembelee jiji la Ouagadougou, Bukina Faso aone jinsi walivyojipanga hata miaka hamsini ijayo basi hakutakuwa na mzongomano wa magari. Maoni yangu ni kuwa serikali ihamie haraka Dodoma. Dodoma mji uwe na "Planning Strategy" ya mji ambao kutakuwa na sera na sheria za kulinda mji zidi ya ufamizi wa ardhi na ujenzi wa kiholela.
ReplyDeleteDar imeanza kujengwa kabla vita kuu ya kwanza kuanza, kwa hiyo kukarabati infastructure za karne ya 19 ili kukidhi haja ya karne ya 21 sio suala la busara. La msingi ni kujenga mji mpya nje kidogo ya mji wa Dar, hasa kwa upande wa kaskazini kwa sababu tunategemea kwamba siku za mbele bandari kuu nchini itakuwa ni Bagamoyo.
ReplyDeleteKama tukifanya hivyo na kuhamishia baadhi ya shughuli muhimu huko pia itasababisha magari mengi kuelekea huko.