Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 32 mpaka sasa

  1. Picha na hali halisi vitu viwili tofauti

    ReplyDelete
  2. Naona michuzi unatuwekea picha za city centre mara kwa mara kwingineko vipi kama tandale, uwanja wa fisi manzese japo tupate kuona barabara zina mashimo na mifereji ya maji machafu

    ReplyDelete
  3. Kuna watu wanajifahamu kwamba si wazuri au warembo lakini wakipiga picha hupendeza na kujishangaa. Hawa wanaitwa photogenic. Dar is photogenic with oblique air photograph!!!

    ReplyDelete
  4. majumba marefu tu , mji hauna huduma za lazima kama maji na umeme, ni sawa na mtu ambaye mrefu lakini kichwani mtupu

    ReplyDelete
  5. Mijitu mingine bana, hawana zuri. wao ni kuwa negative saa zote. inaonekana hata nyumbani kwake akienda chooni na kukuta kusaif atakasirika - kisa? anataka kuona kimba pale juu. acheni hizo watanzania!!!! pia kama unataka kuona mambo negative saa zote kuna mitandao specialist wa kazi hizo. muacheni ankali abaki positive na kudumisha heshima na uaminifu alionao dunia nzima.

    ReplyDelete
  6. Hahahaaaaaaa we mdau hapo juu... mbavu sina. Yaani umeelezea haswa taswira ya Mtanzania mwenye akili kama hao wapondaji wa kiiiiila kitu. Ati akikuta chooni kusafi anakasirika, anataka akute kimba hahahaaaa safi sana Mitanzania mingi iko hivyo, haina zuri na mijuaji balaa.

    ReplyDelete
  7. Hahahaaaaaaa we mdau hapo juu... mbavu sina. Yaani umeelezea haswa taswira ya Mtanzania mwenye akili kama hao wapondaji wa kiiiiila kitu. Ati akikuta chooni kusafi anakasirika, anataka akute kimba hahahaaaa safi sana Mitanzania mingi iko hivyo, haina zuri na mijuaji balaa.

    ReplyDelete
  8. Ukweli ndio huo kubalini tu daa miundombinu zero, kuchafu..no maji nk.!!!! nani asiyependa nchi yake?? ila ukweli utabaki palepale

    ReplyDelete
  9. Ukweli unaujua weye? jitokeze tukuone unakoishi (nyumbani kwako) ndipo ukenue hapa. mkome na mlegee na propaganda zenu za kisiasa. na mtachukia sana!!!

    ReplyDelete
  10. Ukweli unaujua weye? jitokeze tukuone unakoishi (nyumbani kwako) ndipo ukenue hapa. mkome na mlegee na propaganda zenu za kisiasa. na mtachukia sana!!!

    ReplyDelete
  11. Jamani tuwe waungwana kidogo. Nyie mnaosema majumba marefu lakini huduma hafifu, chukulia wewe leo ungekuwa rais au waziri ungetufanyia nini watanzania? kila kitu kinaendelea polepole jamani. Tusitake kujigamba kwa vile tupo nje huku kwa wenzetu kuzuri na tunasahau nyumbani. Tutaendelea polepole tu ila matusi hayatatupa maendeleo hata kidogo. Tuwe watu positive sometimes.

    ReplyDelete
  12. hii ndio bongo tambarare ya kina ras makunja wa ffu? kweli tambarare

    ReplyDelete
  13. Majuzi hapa kuna " Mdau" mmoja alisema watanzania tunaombwa kusifia.

    Nawaza huyu mdau kama kapita hapa leo atatushauri nini? yaonesha wengi tumekataa ombi la kusifia?

    Mdau upo?

    ReplyDelete
  14. Waazaliwa wa jijini akina ras makunja ndio wanaolijua jiji lao la lawama

    ReplyDelete
  15. Duh Kaka!

    Hiyo man dhari kama NYOKO SITI vile!

    Dah!

    ReplyDelete
  16. Watanzania acheni kukosa uzalendo hata huko kwa wabeba boxes kuna sehemu mbovu huwezi kuamini lakini umeshawahi kuona wameweka kwenye vyombo vyao vya habari?.. Tembeeni muone siyo mnakalia kukaa miji mikubwa na kuwa negative kila kitu kuhusu nchi yenu.

    ReplyDelete
  17. Watu mnaongea tu but mna uhakika hiyo ni Daslama???Hapa Ankal Michuzi kawaingiza choo cha kike na nyie mmeingia tu bila kutizama vizuri kama ni daslama kweli au no??basi hio picha sio ya Bongo daslama!!isomeni vizuri.

    ReplyDelete
  18. duu noma mji mpangilio equals to zero

    ReplyDelete
  19. nyinyi mmnaponda dar yenu wa wapi au ndio rudini mkarekebishe bac nchi mmesomeshwa na serikali leo mmakimbia nchi yenu ndio uzalendo au njooni tuunge behewaa kidogo kidogo ili tufikie walau nusu ya reli.

    ReplyDelete
  20. Mdau uliosema dar is photogenic nakubaliana na wewe asilimia 100%, Au labda picha iyo ilikuwa developed kwenye sofware kwa lugha ya kitaalamu ni CITY PLAN SIMULATOR.ambayo upelekea kutokea kwa kivuli ambacho si halisia(yaani Virtual Image).
    Mdau-Australia
    Modelling and simulation software Developer

    ReplyDelete
  21. mdau wa australia kula tano..hii ni simulation..dar original sii kihivyo..hii ni dar ya picha teeehteeh..

    ReplyDelete
  22. Sisi tuko kariakoo hapa chini. Shuka uone

    ReplyDelete
  23. kuna rafiki yangu mmoja aliwahi kuniambia, jinsi unavyozidi kukaa huku ulaya/nje ya afrika ndivyo unavyozidi kuwa bwege sasa naamini.eti jitu linajidai mdau sijui kutoka australia tena software developer halafu ana comment kwa imagination zake.jamani pamoja na kwa mnapiga sana box muwe mnakwenda angalau bongo kutembea muone mji unavyobadilika sio kukaa na kukandia kwamba sijui photoshop,sijui virtual image sijui nini! mnapiga box halafu mnajidai software developer.kwa mawazo hayo nani akupe kazi Australia hii!!!

    ReplyDelete
  24. iyo picha tukisema tui-zoom kila particle,japo basi tupate hata kuona miundo mbinu kule chini, unaweza usiamini macho yako.ni sawa sawa na mtu mfupi kwenye picha kuonekana ni mrefu.pia Mdau uliosema kuhusu simulation inawezekana pia.

    ReplyDelete
  25. Vyovyote ilivyo ila haki lazima isemwe japo inauma, maana haki ndivyo ilivyo! Ni ujinga wa hali ya juu kuwa na jiji kama hili halafu kukosekana kwa huduma mbili muhimu kabisa, MAJI na UMEME. Nani alisema uzalendo ni kukubali kila kibaya. NI aibu kubwa kabisa na tunaipenda nchi yetu ndio maana tunasema hivyo-Mdau Japan

    ReplyDelete
  26. Hata sisi wengine tumeishi nje miaka mingi na tukaamua kurudi nyumbani,ni kweli kuna matatizo ya hapa na pale, ila generally maendeleo yapo...na hii picha sio simulated..it's real!!!,some of you haven't been at home for many years, ndio maana mna-deny facts...tembeleeni muone mabadiliko na mchangie jinsi ya kuendeleza miondo mbinu...sio kuponda tu huku kwenye mitandao...ni sawa na kukimbia kivuli chako mwenyewe

    ReplyDelete
  27. Waacheni wakae naujinga wao wautumwa ulaya mana hata shule hawajaenda nikubangaiza na kuishia michuzi blog wakifiwa utawaonea huruma.......

    ReplyDelete
  28. Maendeleo mazuri sana. Lakini wamebanana sana. Why not expand these beautiful idevelopments - all along the road to Bagamoyo. Town planning is a definite issue. Kuhusu umeme, nahisi kwamba sehemu hizo hazikatiwi. Hizo ghorofa utapandaje bila lift? Umene ukikatwa wakati uko half way up and stuck for possibly hours is just a frightening thought. Na majority of these high rises are offices which use computers. Kutumia generators not cost effective or environmentally friendly. So i conclude that Umeme haukatwi kamwe sehemu hizo. Bahari yetu inapendeza sana as always. Tanzania juu juu juu zaidi.

    ReplyDelete
  29. WADAU WOOTE NIMEWASOMA HAPO JUU.NAONA MNABISHANA NAWENGINE HAWATAKI KUKUBALI UKWELI.EMBU JAMANI WATZ TUWETUNAKUBALI UKWELI NA UWAZI.KUWA MJI UNASIFIWA UMEJENGWA SIJUI MAJENGO MAREFU.UJINGA MTUPU DAR INAONGOZA KWAKUKOSA UDUMA NYINGI SANA ZAJAMII.NAZAMUHIMU.MAJI YASHIDA SAANA.UMEME HAKUNA NIWAMGAO MPAKA LEO HAIJULIKANI SOLUTION LAKE.LAZIMA TUSEME UKWELI SIOKUSIFIA TUU MAJENGO HAILETI MAANA.EBU JARIBUNI KUTEMBELEA KAMA MIJI YA NAIROBI MPATE MFANO MZURI.YAANI HAPO NISAWA NAKUMSIFIA MWANAMKE MZURI SANA KWAMUONEKANO WANJE.TABIA MBAYA UKIENDA NYUMBANI KWAKE KUCHAFU MLEVI NK.SO TUBADILKE WATANZANIA TUKUBALI CHALENGE.SIO KUSIFIA TU KILAKITU FOR NOTHING.JUST SAYING.

    ReplyDelete
  30. Jamani, jamani, jamani, kweli mkataa kwao ni mtumwa! Hii sio 'CITY PLAN SIMULATOR' hii ni picha halisi ya Dar s Salaam ama kwa sababu imechukuliwa kitaalam ndio maana imewachanganya? Hebu msijifanye kuwa Tanzania sio kwenu, mmekaa huko nje mpaka mnakuwa watumwa? Rudini basi angalau muone mabadiliko.

    ReplyDelete
  31. Jamani mbona siye wabongo wanafiki sana?!! Hivi tumelogwa na nani?! Sidhani watu wanaongelea matatizo ya Bongo hawaijui Bongo au wameondoka Bongo basi hawayajui matatizo yake sasa hivi. Nadhani wote tuna lengo moja, tunapenda kwetu, na ndiyo maana mtu anachukua muda wake kuandika lolote hapa. Lakini mtu akikosoa kitu sio kusema kwamba hapendi kwao, bali anataka tujerekebishe. Ni kweli kwa sie tunaoishi Bongo, tena Upanga, maji na umeme ni tatizo kubwa sana. Na hayo majengo mnayesema marefu pale mjini ndiyo kabisa, hayafai. Kuna wakati umeme ulikatika, mie na mke ikabidi tutelemke gorofa kumi na joto la Bongo ni balaa. Tunaona yanavyoporomoka yenyewe. Je ikitokea Sunami au Tetemeko itakuwaje?!!(Mungu atuepushe na haya majanga. Lakini inabidi tujipange wenyewe uku tukimwomba Mungu. Vile vile mvua ikinyesha tunaona miundo mbinu ilivyo mibovu, watu inabidi tukanyage maji ya taka humo humo(nimejisitili kusema k........). Kusema ukweli mie napenda mikoani, Dar nalazimishwa na kazi. Lakini vitu vingine mtu inabidi ukubali ili tujirekibishe kwa manufaa yetu. Mfano, ndiyo mtu unweza ukawa unapenda timu fulani lakini kama ni mbovu inabidi ukosoe tu, ili labda ijipange upya.

    ReplyDelete
  32. jiji la dar linakua kwa kas sana na ktk kum bora ya majengo marefu afrika tz ipo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...