CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimewashukuru Watanzania kwa kukiamini na kukipatia ushindi wa kishindo katika uchaguzi mdogo wa udiwani uliofanyika jana katika kata 27 na CCM kushinda kata 23. 


Akitoa shukrani hizo, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amesema leo kwamba siri ya CCM kuimwaga CHADEMA ni uadilifu katika kuwatumikia wananchi na kwamba, kushindwa kwa chama hicho ni ushahidi kwamba hakikubaliki na Watanzania wamewathibitishia kwamba hawajazoea vurugu.
Nape alisema CCM inaahidi kuendelea kuwatumikia Watanzania kwa amani na utulivu kwa kuwa ina uzoefu wa kufanya siasa kistaarabu na ndio siri ya kukubalika kwa wananchi.
Akizungumzia kushindwa kwa CHADEMA alisema wamehukumiwa kutokana na vurugu na kupiga watu kwenye kampeni za uchaguzi na ndio maana wametumia gharama kubwa na helkopta tatu na kuambulia kata tatu.
"CHADEMA wamevuna walichopanda Watanzania hawapenda vurugu, wamezoea amani na utulivu sasa wamewaadhibu kwa kuwanyima kura na huo ni ushahidi kwamba Watanzania hawakiamini," alisema.

Katika uchaguzi huo CCM ilishinda katika kata 23 za Kibindu na Magomeni (Pwani), Kiwalala na Namikage (Lindi), Ubwage (Shinyanga), Ibumu na  Nduli (Iringa), Kiomoni na Mtae (Tanga), Nyasura(Mara), Malindo, Santillya (Mbeya), Partimbo(Arusha, Mkwiti (Mtwara), Tungi na Ludewa (Morogoro) na Mrijo (Dodoma).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. CHADEMA hawana busara na subra,wanadhani kuzungumza kwa nguvu na sauti kubwa ndio kusikika. Na bado huo ni mwanzo tu. Hatutaki ukimbizi,tumechoka na vitendo vyao vya uchochezi na dharau maana kila mwanachama anajiona anajua. Huku vyuo vikuu wanajiiita intellectuals na ambaye sio chadema humuona hajaelimika.

    ReplyDelete
  2. SULUHISHO NI
    (1)TUME HURU YA UCHAGUZI
    (2) WAFANYAKAZI WOTE WA TUME HURU YA UCHAGUZI WATAKUWA NI WA KUDUMUKUANZIA NGAZI YA KIJIJI HADI TAIFA
    (3) VYAMA VYOTE VIPEWE RUZUKU SAWASAWA ILI KUWEPO NA USHINDANI WA WAGOMBEA ULIOSAWA. KUNA VYAMA VINASHINDWA KUELEZA SERA KUTOKANA NA UKATA. RUZUKU ITOKE MOJA KWA MOJA HAZINA. CHA MSINGI TU PROPER MECHANISM IWEPO.
    (4) KIKOSI CHA ULINZI NA USALAMA KITAKACHOHUSU UCHAGUZI NA USALAMA WA UCHAGUZI NA VYAMA VYA SIASA KIUNDWE NA KIWE CHINI YA TUME HURU YA UCHAGUZI. NA KAMANDA MKUU NI MKUU WA TUME HURU YA UCHAGUZI.

    ReplyDelete
  3. Duh! Kelele zote za Chadema kumbe wamechukua kata tatu tu? Sasa inaingiaje katika akili ya mtu mzima Joseph Mbilinyi au Sugu, kusimama hadharani na kuwaambia wananchi kwamba Chadema wanachukua nchi katika uchaguzi mkuu mwakani? Hotuba za aina hii zinatukatisha tamaa za kuwapa kura.
    - Mr Mhoja - Sweden

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...