Makamu wa Rais Dkt Bilal (katikati) akizungumza na Rais wa Uganda Yower Museven (kulia) kabla ya Mkutano huo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (kushoto) na Makamu Rais wa Burundi Gervas Rufykiri, wakitia saini kushiriki katika mkutano huo.
![]() |
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal (kushoto) akizungumza katika mkutano huo |
Rais wa Uganda Yoweri Museven, akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Nne wa wakuu wa Nchi wanachama wa Ushirikiano wa Kanda ya Kaskazini. Umoja huo unaundwa na nchi za Uganda, Kenya, Rwanda na Sudan Kusini,Tanzania na Burundi zimeshiriki mkutano huo kama nchi waalikwa ambao pamoja na mambo megine waliyojadili ni kukamilisha miradi mbalimbali inayofanywa kwa pamoja na ushirikiano huo.
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo na ujumbe wa Tanzania.
Picha na OMR
Ujirani mwema uendelee.
ReplyDeleteKama Waalikwa !! Dah
ReplyDeleteNi waalikwa kwani kuna jumuia mbili tofauti: EAC na Northern Corridor integration
ReplyDeleteHakuna haja ya kupoteza muda na kujibembeleza kwa watu.
ReplyDeleteSioni sababu ya Tanzania kuhudhuria kama mwalikwa badala ya Mshiriki kamili ktk EAC.
Kama ni suala la Miundo mbinu tufanye mpango mwingine ikiwezekana na nchi kama Congo-DRC, Msumbiji, Zambia na Angola ambazo tuna uhusiano nao hata wa Kiuchumi na zenye tija zaidi kwetu kuliko 'CoW' yule ambaye ni ng'ombe Jini mwenye miguu mitatu badaya la minne anayeweza kufariki muda wowote ule kwanza Marais wake kila mmoja amekalia kutim kavu kwake.
Wake up Tanzania let us find other alternative ways !!!
Bora twende zetu Afrika ya Mashariki ni ya mashaka mashaka!
ReplyDeleteBora tuwapake mafuta kwa mgongo wa chupa!
ReplyDeleteSiri ni kuwa :
1.Hawa jamaa baada ya kututenga wakaja fahamu ya kuwa tuna umuhimu sana kwao kuliko walivyo fikiri hapo kabla.
-Tazameni suala la Single Tourist Visa lipo wapi hadi sasa?,
-Ni kuwa halitekelezeki kwa sababu Rwanda ndio walitakiwa kutoa Stoikcer za Visas hadi sasa wanasuasua na zoezi halijaanza Rasmi kama walivyosema kinachoendelea lina fanya kienyeji tu watu wanavuka holela kwa misingi wa Tamko lao.
-Imesikika huku wengine wakilalamikia Wafugaji 100 wa RWANDA wameingia Uganda wakitumia hizo ID's na mifugo yao huku Waganda wakilalamikia Serikali yao kwa uamuzi huo.
2.Miradi ya Miudno mbinu.
-Mradi wa Reli Mombasa hadi Kigali zinatakiwa USD 13 Bilion,(Kenya 7 Bilion, Uganda na Rwanda 6 Bilion) huku Rwanda na Uganda zikiwa hajijafanya lolote wakti Kenya ikiwa Sualalimeingia kizungu mkuti likipingwa Bungeni kuwa Gharama zimezidishwa kuliko ilivyo halisi hivyo pana pingamizi kusimamisha Mradi kuendele.
-Mradi wa Bandari Lamu ni kuwa Bomba la Mafuta linatakiwa litokee Sudan Kusini wakati hali ikiwa bado ni tete nchi imevurugika kwa Maasi ya Vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Hivyo bora tuwapake mafuta kwa mgongo wa chupa kwa kuhudhuria vikao vyao walivyo tutenga hapo kabla ambavyo mambo mengi ni wazi hayatatimia !
Wanajumuia wa ukweli wamewakilishwa na maraisi!!!!
ReplyDelete