Waziri wa Ujenzi,Dkt. John Pombe Magufuli amesafiri akitokea Mkoani Dodoma anakohudhuria Vikao vya Bunge la Katiba na kwenda moja kwa moja Morogoro maeneo ya Mikese (Kilomita kumi kutoka Mzani wa Mikese kuelekea Dar), ambapo magari mawili yaligongana na kuteketea kwa moto na kusababisha kifo cha mtu mmoja alietambulika kwa jina la Moud Amin.

Ajali hiyo ambayo imetokea mapema leo ilifunga barabara yote ya Dar - Morogoro, takribani kwa masaa zaidi ya mawili na kusababisha foleni kubwa ya takribani kilomita 30. Malori hayo, lori moja lilikuwa likitokea Bukoba, mkoani Kagera likielekea Dar na lori lingine likielekea Sumbawanga, mkoani Rukwa. Chanzo cha ajali bado hakijafahamina na uchunguzi bado unaendelea.

Aidha, Dkt. Magufuli kwa mamlaka aliyopewa, ameruhusu malori yaliyokuwa yamesongamana kupita mzani wa Mikese bila kupimwa ili kuondoa usumbufu mwingine katika mzani wa Mikese.

Dkt. Magufuli kwa pamoja na mhandisi wa mkoa wa Morogoro Mhandisi Tenga walisimamia ukwamuaji wa malori hayo.
Dkt. Magufuli akiangalia hali ya lori hilo mara baada ya kuwasili katika eneo la tukio, Mikese Morogoro.
Dkt. Magufuli akiongea na baadhi ya wahanga wa ajali hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Hon. Magufuli, nafurahishwa sana na jinsi unavyotupa wa-Tanzania utumishi uliotukuka ..... wakati wengine wako kwenye "mjadala wa posho" wewe uko "live" kujua nini kinawasibu wa-Tanzania....sijajua kama wa-Tanzania tunaweza kutoa mchango gani ili kuenzi watumishi kama hawa......viongozi wote dunani waliwahi kupata heshima, hadhi na kuacha "legacy" walijitoa kwa kuwatumikia watu kwa moyo wa dhati ....keep it up, Hon. JP Magufuli.

    ReplyDelete
  2. Mungu azidi kukubariki mheshimiwa umekuwa wa tofauti sana katika watu wanaotuongoza kwenye hii nchi.

    ReplyDelete
  3. Nashkuru sana kuwa Waziri muhusika wa barabara amefika na kujionea hali halisi ya tokeo hili likiainisha na kama hili wiki mbili zilizopita.Waziri Magufuli sasa chemsha bongo lako na ujiulize jee kuna haja ya kuweka mikataba mipya ya kujenga barabara nyingi zaidi bila ya kuweka kipaumbele kwa kona kali au miteremko mirefu bila ya kuitanua kuisawazisha?Ukishindwa na hilo basi ni dhahiri kama haya yataendelea kutokea siku hadi siku.Usijekwepa lawama.

    ReplyDelete
  4. Hon. Magufuli...Lets see your Magic and help saves lives of Tanzanians. Please help stop this carnage on our roads...how can this happen day after day? there is no one who is answerable...hao wenye mabasi, owners and drivers both hawajibiki to any one...I am asking why? especially when so many of us are dying on OUR ROADS?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...