Watu watatu wanashikiliwa na polisi nchini Panama kwa tuhuma za kuhusika na begi lililokutwa na dola za Kimarekani 7.2 (pichani) katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa TocumenJumapili hii, ambapo wapelelezi wanahisi mkwanja huo ulikuwa unahamishwa kutoka Honduras kwa moja ya makundi ya wauza 'sembe'  (madawa ya kulevya) ambalo hawakulitaja. Mkwanja huo zaidi ulikuwa wa noti za dola 100.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Mojawapo wa Makundi maafuru nchi za Marekani Kusini ya Mipango ya Sembe:

    1.Golden Crescent Honduras(Panama)
    2.Meddelin Columbia(Colombia)
    3.Guadalajara Mexicana(Mexico)

    Hawa jamaa Makundi yao ni kama Serikali kamili maana wanamiliki Majeshi wakiwa na Vifaru na Viwanja vya ndege na Makombora ya Kivita, Maabara kubwa za kisasa na Viwanda vya Madawa huku wakiajiri Maprofesa na Madakitari waliosoma sana ktk Taaluma kama Chemistry, Physican Chemistry na Industrial Chemistry.

    Inasemekana wanakoishi hakuna njia za kuwafikia kwa sababu Mashamba ya Sembe yapo juu ya milima na yemezungukwa na misitu minene sana usafiri wa kufika huko ni kwa njia ya ndege tu!

    ReplyDelete
  2. Jamaa hapo juu kanifurahisha sana ,paragraph ya mwisho kasema " inasemekaka hakuna njia za kuwafikia" lakini hapo hapo anasema "usafiri wa kuwafikia ni kwa njia ya ndege tu" hapo sijui mimi ndo sijaelewa au yeye ndo kanichanganya?!simulizi nzuri lakini mhmm haya nanyie msome.

    ReplyDelete
  3. Mdau wa 2 Mdau wa kwanza amemaanisha ya kuwa kutokana na Msitu mzito ulio zunguka mashamba ya mazao ya sembe hakuna Njia za Barabara za magari ardhini kuwafikia bali ni kwa ndege tu!

    ReplyDelete
  4. Pana Genge lingine linaitwa CALI CARTEL (hili halina nchi moja na haijulikani Makao Makuu ni wapi ama nchi gani na Kiongozi Mkuu ni nani)

    Wapo wanaohisi kuwa Makao Makuu ni Panama kwa aliyekuwa Raisi wa nchi hiyo General Manuel Noriega aliye kamatwa na kufungwa Florida nchini Marekani na Marekani mwaka 1989.

    ReplyDelete
  5. Pana Makundi haya (Cartels) huko nchini Mexico jirani na maeneo ya huko huko Panama, kwa kuwa Drug ni bidhaa inayo tegemea supply chain ktk Mfumo wa Masoko unaweza kukuta Mzigo huo wa Pesa ulikuwa ni mauzo ya Sembe na ulikuwa unasafirishwa na Makundi ya nje ya Panama ya nchi kama Mexico:

    Mkundi ya Sembe hatari Mexico:

    1.Beltrán Leyva Cartel
    2.Michoacan drug cartel
    3.Knights Templar drug cartel

    Tazameni link hii wanapoikuwa Kazini wauza Sembe ni kama vita vile?

    https://www.google.co.tz/search?q=mexico&ie=utf-8&oe=utf-8&rls=org.mozilla:en-US:official&client=firefox-a&channel=fflb&gws_rd=cr&ei=-zP6UpumLNGIhQfnuYDwBw#channel=fflb&q=mexico+drug+cartels&rls=org.mozilla:en-US:official

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...