Mwenyekiti mpya wa TAHA, Bw. Eric Ng'imaryo, akizungumza mara
baada ya kuchaguliwa kushika wadhifa huo.
Na Mwandishi Wetu
TAASISI inayoshughulika na kilimo cha maua na mboga mboga nchini
(Tanzania Horticultural Association -TAHA) imemteua Bw. Eric Ng'imaryo kama Mwenyekiti wake mpya kuchukua
nafasi iliyoaachwa wazi na Bw. Colman Ngalo, ambaye ameiendesha
taasisi hiyo kwa mafanikio kwa takribani miaka kumi ya utawala wake.
Sambamba na uteuzi huo pia Bw. Ng'imaryo.
Pia taasisi hiyo imepata
Makamu Mwenyekiti mpya pamoja na wajumbe wanane wa Bodi ya TAHA pia
walichaguliwa katika Mkutano Mkuu uliofanyika hivi
karibuni jijini Arusha.
Miongoni mwa wanaounda Bodi mpya ya taasisi ya TAHA ni pamoja na: Bi.
Fatma Riyami, Bw. Ravi Bhalerao, Bw. Herald Peeters , Bw. Juma
Lossini, Bw. Robert Daniel, Bw. Tjerk Scheltema na Bw. Adrian Moss.
Bw. Eric kwa kuchaguliwa kwake kuwa Mwenyekiti wa Bodi mpya ya TAHA na
ni mategemeo yangu kuwa tutaendelea kufanya kazi pamoja naye katika
miaka ijayo.
Mchanganyiko wa ujuzi wake katika sekta ya maua na mboga mboga na
uzoefu mkubwa sambamba na utaalamu unafanya kuwa mtu bora kuchukua
nafasi ya Uenyekiti wa TAHA na sekta yenye maendeleo endelevu.
"Napenda pia kuishukuru Sekretarieti ya TAHA na wanachama wake kwa
ushirikiano wao bora katika muongo uliopita. Kwa ushirikiano tumepata
mafanikio mkubwa. Mimi ninajisikia fahari kubwa kukabidhi taasisi hii
yenye mafanikio ambayo bado ina fursa kubwa kwa ukuaji zaidi katika
TAHA na sekta nzima kwa ujumla."
TAHA ni taasisi ambayo ni mwanachama wa sekta binafsi ambapo imekuwa
ikishiriki kwa ufanisi katika kubadilisha kilimo cha sekta ya maua na
mboga mboga toka kuanzishwa kwake mwaka 2004.
Kutokana wa hatua za uwepo wa TAHA , sekta ya maua na mboga mboga
nchini na kufanikiwa kuvutia washirika mbali mbali kutoa misaada
mikubwa ikiwa ni pamoja na serikali ya Tanzania na Washirika kama vile
USAID, BEST- AC, Ubalozi wa Uholanzi , ITC, na Serikali Finland.
TAHA inatoa sapoti mbali mbali kwa wadau wa sekta ya maua na mboga
mboga ikiwemo kuwajengea uwezo kwenye majukwaa, kulinda na kukuza
maslahi ya watendaji katika sekta hiyo ya maua yaani wazalishaji,
wauzaji, wasindikaji, na watoa huduma ya maua, matunda , mboga,
viungo, mimea na mbegu za maua
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...