Katika kushangaa
wingi wa askari hawa, nilimekua nikihesabu makundi ya askari wa usalama barabarani
ambayo yanafika zaidi ya nane (hii ni kutoa walioko mizani Kibaha). Kuna sehemu
ya kipande cha umbali wa kama 5km unapotokea Kongowe kwenda Mlandizi, kunakua
na polisi makundi hadi manne walioko umbali wa chini ya 2km kutoka kundi moja
hadi jingine.
Vituo hivi
wanaposimama polisi, kuna askari zaidi ya wawili na kuna kundi linakua na askari hadi sita. Kwa hali hii
unaweza kujikuta unasimamishwa kila baada ya 2km au 5km na kila unaposimamishwa
wote wanauliza mambo yaleyale; wanakutaka uoneshe leseni yako, kadi ya gari,
fire extinguisher, kukagua bima na road license. Kibaya zaidi ni kuwa hakuna
uratibu au mawasiliano yanayoweza kukufanya ukikaguliwa kituo hiki usikaguliwe
kinachofuata. Hivyo unaweza kunajikuta unasimamishwa na kuulizwa mambo yaleyale
na kukaguliwa vitu vilevile kila baada ya umbali mdogo sana.
Mazingira ya barabara
hii na wingi wa magari haviruhusu sana dereva kukimbiza gari kwa mwendo wa
kutisha. Lakini kuna makundi kadhaa ya askari hawa wenye tochi za kupima
mwendokasi na wanafanya hivi kwa kujificha au kuvizia.
Kwa mtazamo wangu,
huu mpangilio au matumizi ya askari unahitaji kutizamwa upya kwa sababu
zifuatazo:
1.
Moja; ninaona kama haya
ni matumizi mabaya ya nguvu kazi na rasilimali watu. Kuweka kundi kubwa namna
hili la askari wa usalama katika umbali mdogo kiasi hiki ni kutumia rasilimali watu
vibaya. Ni gharama kubwa sana kuajiri watu na kisha kukawa hakuna kazi ya
kutosha kufanya na kufanya kazi ya mtu mmoja kuwa ya watu kumi.
2.
Mbili; Askari hawa
wanatumika kwa wingi hivi sehemu moja wakati ni kweli kuwa kuna uhitaji mkubwa
sana wa ulinzi na usalama kwenye maeneo mengi wanayoishi raia. Ninadhani ndugu
zetu hawa wangeweza kutusaidia usalama maeneo mengi mengine na tukawa na jamii
ambayo iko salama na amani zaidi ya ilivyo sasa
3.
Tatu: Ninaona kama huku ni
kutesa raia na waendesha magari pale ambapo gari linasimamishwa kila baada ya
muda na umbali mfupi na kuulizwa maswali yaleyale na kukaguliwa vitu vilevile. Katika
kupita njia hii na kusimamishwa kwenye umbali usiozidi 2km, niilimuuliza askari
mmoja ni kwa nini wana utaratibu mbaya hivyo; naye akakiri kuwa ni mfumo mbaya
na anaomba tushauri njia mbadala.
4.
Nne, kwa mtazamo wangu, hali
hii inachelewesha sana maendeleo na kuongeza umaskini kwa nchi yetu. Tayari tuna
tatizo kubwa la matumizi ya muda ambalo linachangia sana umaskini katika nchi
yetu. Kulazimishwa kupoteza muda zaidi bararabara kwa mambo yasiyo na tija ni kushindwa kuthamini matumizi sahihi ya muda
kama kiungo muhim sana cha maendeleo binafsi, familia, jamii na taifa
5.
Tano; Askari wengi hawana
haraka na hawaogopi kukupotezea muda wapendavyo. Unaweza kusimamishwa ukiwa na
kila kinachotakiwa na bado ukajikuta unapotezewa muda tu na mara nyingine
kuambiwa unapelekwa kituoni kwa jambo ambalo halina ulazima huo. Wengi wa
askari hawa wanashikwa na hasira wanapokukuta huna kosa.
Ushauri kwa Jeshi la Polisi:
1. Jeshi la polisi na seriakli kwa ujumla, liwekeze zaidi
katika kutoa elimu sahihi ya usalama barabarani ikiwa ni pamoja na kudhibiti
upatikanaji wa leseni bila mafunzo, ili kuhakikisha kuwa watumiaji wa barabara
wana elimu na ufahamu wa kutosha kuhusu matumizi ya barabara na hivyo kuondoa
ulazima wa kutumia nguvu kubwa kusimamia sheria
2. Jeshi la polisi wajisikie vibaya kujenga kizazi na jamii
inayotii sheria kwa woga na shuruti na badala yake ifurahie kuwa na jamii
inayotii sheria kw akupenda. Kwa minajili hiyo, isiwekeze sana katika kutoa
adhabu na kuvizia makosa ya kuadhibu, bali wawekeze katika kuelimisha, kuelekeza
na kuongoza.
3. Kuna haja ya ungozi wa jeshi la polisi kushirikiana na
wataalamu wa fani zingine kama ICT kuangalia namna nzuri, rahisi, ya kisasa na
yenye gharama nafuu katika kufanya ukaguzi wa kawaida wa magari barabarani. Kwa
mfano, kwa magari yanayokwenda mikoani (hasa madogo) kunaweza kuwekwa utaratibu
kuwa, likashakaguliwa mambo ya msingi katika kituo cha kwanza (mfano kikawa
baada ya mbezi mwisho), kunakua na alama inayoonesha gari na dereva wana vigezo
vya kutembea njia kuu bila ukaguzi hadi mwisho wa safari; isipokua tu iwapo
atatenda kosa. Hili linawezekana kabisa ikiwa ni pamoja na kuwawezesha askari
wa vituo vingine kuhakiki (validate) ukaguzi husika.
4. Pamoja na unyeti wa kazi za walinzi hawa wa usalama wetu,
ni vema wakatambua umuhimu na unyeti wa muda katika kulitoa taifa letu hapa
lilipo. Ni shida kidogo unapokwenda umbali wa 50km na kutumia masaa kadhaa kwa
sababu tu ya ukaguzi wa kila hatua chache au kwa sababu askari fulani
alijisikia vizuri kukuonesha mamalaka yake kwa kukuweka barabarani muda mrefu
au kukupeleka kituoni bila kosa
5. Polisi wetu watambue kuwa karne ya watu kujazana Dar es
Salaam imepitwa na wakati. Ni wazi kabisa kuwa kwa sasa baadhi ya watu wanaweza
kufanya kazi au shughuli zao za kipato DSM na wakaishi nje ya mji kama vile Kibaha,
Mlandizi, Ruvu, Bagamoyo, Msata Chalinze na hata Morogoro. Hii inasaidia
kupunguza msongamano ndani ya mji na kuwawezesha watu kufanya shughuli zingine
za uzalishaji hasa kilimo ambacho ni ngumu kufanya hapa mjini. Kwa mfumo wa
kupotezeana muda barabarani ulioko sasa, hili haliwezekani; sio kwa vile maeneo
haya ni mbali sana au kuna foleni; bali ni kwa sababu ya ukaguzi wa polisi
ambao ungeweza kuboreshwa na kuokoa muda.
6. Jeshi la polisi lishirikiane na wataalamu wengine nje ya
jeshi lao kuona namna ambavyo watasimamia sheria na taratibu za barabarani kwa
rasilimali watu ndogo (askari wachache) na bado wakafanikisha majukumu yao kwa
ufanisi mkubwa. Hii haitaondoa tu usumbufu na matumizi mabaya ya rasilimali
watu na muda, bali itapunguza hata shutuma na rushwa zinazohusishwa sana na
askari hawa (bila kujali ni za kweli au uongo)
Mwalimu MM
UDSM
Naunga Mkono hoja hii...kwa kweli ni kero sana kuendesha gari kati ya DSM na Chalinze...checkpoints zimezidi na muda mrefu sana unapotea...hii inaonekana ni njia ya ulaji iliyotengenezwa kwa makusudi kuwanufaisha askari
ReplyDelete