Kwa wale munaokwenda bucha kununua nyama munaelewa ni kwa jinsi gani nyama imepanda bei. Kwa sisi tunaogetemea bucha za maeneo ya Mwenge, tangu nyama ilipopandishwa bei mwezi December mwaka jana wakati wa sikukuu, hadi sasa haijashuka. Kilo moja ilipanda kutoka shilingi 5,000 hadi shilingi 7,000 huku stake ikipanda kutoka shilingi 6,000  hadi shilingi 9,000.
Pamoja na maumivu haya ya bei, kuna maumivu makubwa wanayopata wanunuzi wa nyama (hasa eneo hili la Mwenye) bila kujua kwa njia kuu mbili:
        *Moja ni kutobandikwa kwa bei ya nyama dukani na hivyo unapokuja kununua wakati wa kulipa wanakusoma iwapo unajua bei halisi au la na wanakupa bei ambayo sio halisi ukidhani ndio bei iliyoko. Wanakugundua zaidi pale utakapouliza bei kwa aina ya nyama unayohitaji.
       * Njia ya pili na kubwa zaidi, baadhi ya bucha zilizoko pale zina mizani hii inayoonekana nzuri na ya  kisasa (kwa viwango vya Mwenge) kutokana na u-digitali wake. Hata hivyo mizani hii inatumika na wingi wa maduka haya ya nyama kuibia wateja kwa kiasi kikubwa sana bila wao kujua.
Mizani hii inatakiwa ipime nyama ama ikiwa na sinia (kibebeo) kilichoko juu yake au pasipo kuwa nayo kulingana na unachopima. 

Hata hivyo, kwa vyovyote vile hapo kwenye weight inatakiwa isome 0.00 kabla ya kupima. 
Iwapo katumia Sinia inayoonekana kwenye picha kwa ajili ya kuwekea nyama, anatakiwa abadilishe calibration ili uzito wa sinia usiwe sehemu ya uzito unaopimwa. Hiyo sinia peke yake ina gramu 300 hadi 350 ambayo ni 1/3 ya kilo (zaidi ya robo kilo).
Wajanja hawa wa Mwenge kwa kuwa waanajua kuwa wengi hawana utaalamu wa vipimo, huwa wanaseti mizani kupima 0.00 kabla ya kuweka sinia na anapokuja kuweka sinia na nyama, ina maana nyama unayopewa ina gramu 700 au 650 badala ya 1000 kwa maana ya uzito wa kilo moja.
Kwa kua mara nyingi ninatumia maduka haya, nimekutana na cases ya wizi huu kwenye bucha zaidi ya nne. 
Niliibiwa mara moja na tangu hapo nimekua nikiwakamata mara zote wanapoanza kupima na kuwataka waweke mizani sawa. Huwa wanashtuka sana wanapoona unaelewa kinachoendelea. Jana jioni nilipoona nimefanyiwa hivyo kwenye duka la tano nikaona ni vema nipige picha na niwashirikishe wanunua nyama (sio lazima uwe mlaji) wengine ambao huenda udanganyifu huu umewatafuna mara nyingi bila kujua.
Huku ndiko nchi yetu inapokwenda...watu wengi bila hofu ya Mungu mioyoni mwao wanajitahidi kula kwa nguvu na kwa wingi iwezekanavyo hata kuliko urefu wa kamba zao. Hii ni mbaya sana na inaongeza mzigo kwa mwananchi ambaye tayari analemewa na mizigo ya aina nyingi.

Hivi cases kama hizi mtu anatakiwa kwenye kutoa taarifa za malalamiko kwa nani?

Mnunua Nyama

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 28 mpaka sasa

  1. kww nn usiripoti polisi wakachukuliwa hatua na zipo taasisi zinaowasimamia zionapo malalamiko hayo zichukue hatua

    ReplyDelete
  2. Si lazima ununue hapo njoo huku kwetu Gongo la Mboto kilo shs 4500 nyama safiiii. Hapo bei juuu sababu ya hizo mbwembwe za mataa na mizani ya kisasa. Na wamekwisha wajua ninyi ni matawi ya juu mnakufa tai shingoni.

    ReplyDelete
  3. nashukuru sana mkuu kwa kutuelewesha

    ReplyDelete
  4. Asante mnunua nyama kwa kujali wenzako, tukiamua kushirikiana na kupata ushirikiano usio wa kifisadi na mamlaka husika inawezekana kutokomeza upuuzi huu na mwingine.


    sesophy

    ReplyDelete
  5. Free market? Shop around, there is no monopoly of butchers

    ReplyDelete
  6. Yaani we acha tu tunashikwa kila mahala sijui tutakimbilia wapi vyakula vinapanda bei kila siku na hatulalamiki umeme ndo usiseme jamani hali ni mbaya kweli watanzania hatuna amani tuna uwoga tunaogopa kuandamana

    ReplyDelete
  7. Nimependa unavyotumia lugha ya Kiswahili. Nadhani kesi hii ingepelekwa kwa watu wa viwango kwa vile wao ndio wahusika wa viwango vya bidhaa mbalimbali. Nadhani wanaweza kuweka viwango vya vipimo vya bidhaa, sinauhakika lakini...........

    ReplyDelete
  8. Hizo issue zinazohusu mizani na vipimo zinashughulikiwa na wakala wa vipimo na mizani Tanzania, WEIGHTS AND MEASURES AGENCY (WMA). Wakala hawa wanaanzishwa chini ya sheria halali ya bunge; sheria nambari 20 ya 1982 kama ilivyorejewa mwaka 2002. na hii ni miongoni mwa kazi zao. Kutokana na sheria hii vipimo vyote (mizani) inatakiwa kuwa approved without such approval it is an offence to use them. next time you go ask them if their weights areapproved and stamped and threaten to report them to the agency. angalia watavyoruka.

    ReplyDelete
  9. WAPO WANAOHUSIKA NA UKAGUZI WA MIZANI LAKINI KAZI HIYO WAMEWAACHIA WAUZA NYAMA WENYEWE!

    ReplyDelete
  10. Asante sana ulieleta taarifa hii ...jana tu nimetoka kuyaona haya nyama iliyonunuliwa hapo ilikua pungufu kwa kuangalia tu...nadhan ukinunua kilo nyingi zaidi unaibiwa zaidi...nlitamani irudishwe lakini sababu ilishafika nyumbani ushahidi ungekosekana.ni kweli sio monopoly market lkn kwa taarifa hizi kua na wengine wamegundua hilo itatusaidia kuhama bucha hizo kwa uhakika yaan sio guess work but confirmed facts.siku njema.

    ReplyDelete
  11. Asante sana kwa kutushirikisha hili, nadhani wizi huu uko sehemu nyingi tu siyo tu hapo Mwenge.Mara kadhaa nilihisi nimeibiwa ingawa sikuwa na ushahidi.

    Umefanya vyema kutushirikisha maana mpaka watu wa mizani na vipimo waje wa rekebishe ni leo! walau wenyewe wananchi tukijua kinachoendelea tutakuwa makini na kuhakikisha hatuibiwi.

    ReplyDelete
  12. Tunashukuru sana kwa taarifa hii mm ni mkazi wa kimara kule ndio usithubutu kwenda kununua nyama mizani yao yameichakachua robo kilo nzima, ukinunua nyama kilo 1 hesabu umenunua kilo 1 kasoro ni kidogo sana.

    wamekosa utu kabisa

    ReplyDelete
  13. Hapa mwenge ni shida,Mie Jana nimenunua samaki nikahisi nimepunjwa ila nikaondoka tu,ila kwa taarifa hii umenifumbua macho

    ReplyDelete
  14. Jamani hapa mwenge ni shidaaaa,asante kwa taarifa maana tumeshaibiwa sana na hawa wenye mabutcher

    ReplyDelete
  15. Kama mnaweza, jitahidini kununua nyama pale Ubungo Oilcom petrol station. Lile butcher ni waaminifu sana, wana nyama nzuri na lugha nzuri pia. Nadhani is the best in Dar.

    ReplyDelete
  16. Inawezekana WANAOIBA hawajui kama WANAIBA. Inabidi kuwafahamisha kwanza kuwa WANAIBA

    ReplyDelete
  17. Hapo sinia haitakiwi. Anatakiwa aweke nyama yako kwenye mfuko wa platiki ambao hauna uzito wa kuonyesha. Hata hivyo Bongo maisha poa Steak £3, hapa UK £7. Nataka kurudi Bongo nimeshapata PhD, niwaache hapa walala hoi wa UK wasio na elimu, kazi uongo tu na kumuamubu mzungu ili asiwarejeshe makwao!!

    ReplyDelete
  18. KWELI MDAU UMNAIBIWA MAANA HIYO SINIANI YAKE KIBINAFSI HAIRUHUSIWI KUTUMIA HIYO ANATAKIWA KUWEKA KARATASI MAALUM ZA KUPIMIA NA KUFUNGIA HIYO NYAMA SIO SINIA NDIO SHERIA NA UKIANGALIA YEYE ALIVYOUZIWA HUO MZANIA HAIKUWEPO HIYO SINIA PIA NI UJANJA WAKE MWENYEWE HUYO,SERIKALIJUKUMULENU HILO KUKAMATA MWIZI

    ReplyDelete
  19. Yaani mimi nilikuwa nashangaa mbona nikununua nyama Mwenge inakuwa kidogo au samaki!!! leo umenipa ufumbuzi bora Ubungo pale Oilcom

    ReplyDelete
  20. Wizi mwingine pale Mabucha ya Mwenge ni unaponunua kuku, ukiwapa wakukatie utakuta paja au kiungo kingine kizuri hakipo kumbe wamekidondosha chini na wanakufungia kwa haraka haraka mnoo...pale unapofika nyumbani ndo unatambua hayo yote

    ReplyDelete
  21. asante sana mdau kwa kutujulisha. sisi wa mizani na vipimo tuko katika mchakato wa kufanya kongamano la kitaifa ili kujadili tatizo hili sugu. siku za karibuni tutaanza kutoa semina elekezi kwa wauza nyama wote na kusambaza vipeperushi kwa wananchi ili nao wajue haki yao. ukiwa na malalamiko yako usisite kututembeleaofisi zetu au kutuandikia barua kwenye sanduku letu la posta!!

    ReplyDelete
  22. Frida wa MwengeFebruary 06, 2014

    Yaani jamani ni kweli kabisa hawa watu wa mabucha ya mwenge ni wezi ajabu. Mimi waliwahi kuniibia nilipowashtukia wakaniambia acha watu wengine watakuja nununa na tutawapiga. Kweli hawa watu wanaohusika na hii kazi ya kukagua mizani wanafanya nini? Unanunua kilo tano lakini ukifika nyumbani unagundua ni kilo tatu au tatu na nusu. Jamani hili jambo lifanyiwe kazi. Tunaomba jamani tunaumia kila kona.

    ReplyDelete
  23. Tunashukuru mdau kwa kutushirikisha katika mada hii..i think from now onwards kuibiwa nyama kwa mtindo huu utakuwa umefika kikomo kwangu..Bongo tunaumia kila mahali..

    ReplyDelete
  24. Tunakushukuru sana mdau kwa taarifa ya utafiti wako ambayo kwa kweli itaelimisha wengi sana. Jamani Wakala wa Vipimo hata wangekuwa na wakaguzi elfu 10 hawatatosha kubaini wajanja wote hapa nchini. Hivi karibuni tuliona walivyofanya operesheni za kishtukiza za kukagua mabucha jijini Dar na wakasema wamegundua kuwa wafanyakazi kwenye mabucha hawalipwi mishahara na matajiri wao na ndio chanzo kikubwa cha udanganyifu huu makubwa kwenye mabucha. Hivyo pamoja na kuendelea kufanya kaguzi hizo za kushtukiza, pia wameitaarifu wizara ya kazi na ajira itoe mwongozo kwa wamiliki wa mabucha kuhusu mishahara ya wauzaji wa nyama. Ufumbuzi mkubwa na wa haraka kwa tatizo hili sugu ni kama hivi kupeana taarifa kwa njia mbalimbali kama blogs ili wananchi tuweze kujihami tuendapo bucha kununua nyama. Mdau wa WMA.

    ReplyDelete
  25. Ninashukuru sana mdau huyu kuileta mada hii ya kuibiwa nyama pale Mwenge. Mimi niliwagundua kitambo kabisa. Tena mzani wakati huo ulikuwa tofauti, sio wa digitali. Nilipunjwa kiasi kikubwa na nilipokwenda kupima sokoni, nao walinithibitishia kuwa nimeshaibiwa nyama. Nilipima pale Mwenge sokoni. Niliirudisha sawia nao wakaipokea bila ubishi. Niliwaambia sihitaji tena kwani nilisikitika sana kwa jinsi walivyonipunja kilo nyingi kwenye kiasi nilichonunua kwa ajili ya familia yangu. Walikuwa tayari kuiongezea, lakini nilibadili mawazo kabisa na niliwaambia ni mwisho mimi na rafiki zangu kwenda Mwenge kwa kununua nyama. Nilihamia New Zanzibar Butchery, pale Ubungo Oil Com Petrol Station. Hawana tabia hii ovu ya kuibia wateja. Pia lugha nzuri na nyama safi kila siku.
    Upo wizi kwenye ujazo wa unga wa sembe Kilo 25 kwa bei za jumla. Kwa wale wanaopenda kupokea bei poa, utakuta ujazo sio kilo 25, bali pungufu. Nao tuwe macho na wachuuzi wenye uroho wa aina hii. Unaweza kukuta kilo 20, au 21,22,23,24 kwa udanganyifu kwamba ni kilo 25 kama ilivyoandikwa kwenye mifuko iliyochapishwa. Huu ni wizi kama wizi mwingineo popote. UAMINIFU HUIWEKA NAFSI YAKO HURU. Kwa nini tuumizane sisi kwa sisi? Tujitahidi kuupunguza ugumu wa maisha kwa kuwatolea taarifa wahalifu hawa kwa mamlaka za Vipimo, ujazo na hata polisi kwani inasaidia kupunguza ugumu wa maisha.
    Wengine ni maduka ya kutolea dawa za Mfuko wa Bima ya Taifa ya Afya (NHIF). Sehemu mbali mbali wanawasumbua wadau wa huu mfuko bila kuwapa dawa. Utadhani unapata bure wakati tayari wamewekeana makubaliano ya hiari kutoa huduma ya dawa. Ninaamini kwamba watu wengi hupoteza maisha kwa kutopewa dawa ili hali dawa wanazo madukani mwao. Wengine wanadiriki kusema, NHIF wanatoa malipo pungufu,wakati serikali imeshatangaza rasmi k.m ALUU dawa za malaria zipatikane kwa bei ya wastani Tshs. 1,000/=. Wao wenye maduka hudai kwa visingizio lukuki kwamba ni tshs. 5,000/=.Tuwe na tabia kuwatolea taarifa ili warekebishwe na maafisa wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF). Nimejaribu na wakaonywa. Pia walirudisha fedha taslimu nilizotoa mfukoni kulipia dukani. Maduka matatu tofauti yaliyoidhinishwa waliniambia hawana ALUU za kunipatia. Nilipotambua ni kukwepa Bima, nilianzia kusema ninanunua kwenye duka jingine bila kutanguliza fomu ya Bima. Ndipo nilipodai resiti ikawa kithibitisho. Nilipotoa taarifa ofisi za Mfuko wa Bima ya Taifa ya Afya (NHIF) walinisaidia tukaenda kuwaona wale walioniuzia dawa. Ndipo haki ikatendeka kwangu.

    ReplyDelete
  26. Lakini mbona kwa sinia bila ya kuwa na NYAMa, mizani inasoma 0. Kuna tatizo gani? Nadhani watakuwa wamefanya 'calibration' na kuset ZERO reading kulingana na masi ya sinia. Tuache kulalamika tu bila sababu.

    Wenu, Muuza NYAMA maarufu; asiyeiba.

    ReplyDelete
  27. Mdau wa 5 what do you mean by free market!!!! Kuibia watu kwako ni free market siyo!! Au nawe ni muuza nyama wa mwenge??!!

    ReplyDelete
  28. Mdau uliyesema mizani mbona inasoma zero...soma tena vizuri nilichoandika.

    Sijakurupuka kuandika hili bila utafiti. Na umeona experience watalizozitoa kwa tatizo hili.

    Nimepiga picha kusaidia watu kuelewa ninachokimaanisha na ilikua ni baada ya kuwakatalia kuniibia...na nilipiga wahusika wakioniona wala sikujificha.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...