IDADI kubwa ya Wakazi wa jiji la Dar es Salaam wametoa ushauri kwa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka kulialika kundi la Ambassadors of Christ ‘Kwetu Pazuri’ katika tamasha la mwaka huu.
Wakazi hao walitoa tamko hilo hivi karibuni wakieleza kwamba kundi hilo ni kundi pendwa kwa mashabiki na wapenzi wa muziki wa Injili hapa nchini kwa sababu ya nyimbo zao kukonga nyoyo za mashabiki na wapenzi wengi zaidi.
“Msama Promotions, watuletee Kwetu Pazuri, kwani ni kundi ambalo lina mashabiki na wapenzi wengi ambao wana mashabiki na wapenzi wengi hapa nchini,” alisema mmoja wa mashabiki wa kundi hilo hapa nchini.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Msama Promotions, Alex Msama masuala yote yako kwenye taratibu za kupigiwa kura kupitia mashabiki na wapenzi wa muziki huo hapa nchini, huku wakisubiri taratibu za kupatikana kwa kibali cha tamasha hilo.
Msama alisema tamasha la mwaka huu masuala yote yanayohusiana na Tamasha la Pasaka wanawakabidhi mashabiki na wapenzi wachague kupitia mfumo mpya wa upigaji kura kupitia ujumbe mfupi wa maandishi ‘sms’.
“Mashabiki na wapenzi wakae mkao wa kula kwa ajili ya kupiga kura kusaka mikoa, waimbaji na mgeni rasmi katika tamasha la mwaka huu,” alisema Msama.
Hawa wanyarwanda nimewasikiliza wanaimba vizuri
ReplyDelete'KWETU PAZURI' Wana Injili kutoka Kigali wana tueleza lakini Raisi wao PK mgogoro!
ReplyDeleteAma kweli ndio maana penye familia na watu wa dini utakuta pana mmoja wa wana familia atakuwa Pusha atakuwa Mwuza ama Kibaka!
Sawa Kwetu pazuri !
ReplyDeleteNi vema pia ili pazidi kuwa pazuri mumshauri Raisi wenu aikatae vita na mauaji ya Wapinzani wake ndani na nje ya nchi ya vilima na misitu ya manyani na ardhi yenye rutuba!!!
Wana Injili mnahubiri vyema lakini ni Maajabu ya Musa kuona katika hii Afrika Mashariki yetu yenye 'KWETU PAZURI' tunakuwa na Maraisi wapenda Mauaji na vita, kwa nini tusiwaelekezee Maneno ya Injili waache?
ReplyDelete