President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete  with CCN's Reporter  Christiane Amanpour during an exclusive interview at CNN's London Studios. During then interview on Illegal Wildlife Trade, President Kikwete described it as "Madness and a very serious matter," that calls for joint efforts  to end the bloody trade.President Kikwete was in London to attend the "London Conference on Illegal Wildlife Trade."
Photos by Freddy Maro video Courtesy of CNN
 Thank you for your time , Mr President...
Same to you Christiane...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. Kaka Michuzi Ankal!

    Nimekuvulia kofia wallahi! Hii kitu nilikuwa nasaka kila media hapo Bongo sijaona. Naona wengi, kama sio wote, wamelala fofofo saa izi.
    Nafungua kwako nakuta kitu na boxi!
    Dah! Na Prezidaa kamwaga ukweli mtupu. Naona kina Msigwa m..vi debe saa hizi na usaliti wao. Wenyewe wanadhani sifa kuipakazia nchi yao, kumbe ndio kwanza wanadharaulika. Hongera ankal. BIG UP JK!!! Yaani maraisi karibu 40 ni wewe pekee umechaguliwa kuongelea swala hili. Na hii aidia yako JK ya kupiga marufuku meno ya tembo kuuzwa ndio mwisho wa matatizo. BIG UP MKWERE WETU!!!

    MDAU DUBAI

    ReplyDelete
  2. Naunga mkono hoja ya mdau wa Dubai hapo juu. Nyie Daily Mail mnaona uandishi huo? Sio mna-copy na paste mambo ya watu kama Msigwa ambaye kaishiwa hoja (na jimbo linamtoka hilo la Iringa). What kind of journalism are you engaged in Daily Mail? Why didn't you take the trouble to balance your story and resorted to hanging on one-sided thrash? Shame on you. Now see how credible news media are defacing your shameful reporting on the issue? And yes, to your chagrin, President Kikwete not only shook hands with all and sundry at Lancaster House today. His back also got patted too! Need i say more?

    ReplyDelete
  3. I really liked his response on homosexuality - simply "our people are not ready to even consider what the West is doing." Nci maskini zinatakiwa kuiga mambo ya maendeleo kutoka "West" lakini siyo ...

    ReplyDelete
  4. Lakini mwisho wa siku ukweli utajitenga.Mwinyezi Mungu Mkubwa!

    ReplyDelete
  5. Kwa kweli hali ni mbaya ya kiuchumi lakini mheshimiwa amejibu vizuri Ukweli anajua mungu.

    Well done Mr President on a Gay issue! We are not ready for such called civilisation..

    ReplyDelete
  6. Hongera sana JK kwa majibu mazuri ambayo yalilenga moja kwa moja kwenye issues.

    Na kuhusu gay rights ijapokuwa alikuchomekea lakini umejibu sawa sawa kiilivyo mzee.

    ReplyDelete
  7. Salaam wadau,
    We dont need to hit the bush we have to go straight to the point. Gay issue President amejaribu kurithisha wafadhili kwa kutupa jukumu kwa wananchi Ila ukweli ni kwamba is not our customer value and as well most of our citizen they have there religious value as well so no room for that at all unless otherwise thing change but kwa ujumla Chief amejibu vizuri sana mwaswali especially on human right Nampongeza Rais na pia namuomba sana atengeneze ukaribu na wananchi wake Kwani kesho ataulizwa kwa kila alilolitenda. Amakweli mfalme kuiona pepo ya Mungu ni Kama Ngamia kupita kwenye tundu ya sindano. Maana ni rehma za muumba tu zitakazo msaidia nasi tunamuombe Rais wetu wa sasa na walio tangulia Mungu awape hekma na busara kwenye maamuzi yao.

    ReplyDelete
  8. Amenifurahisha sana Mr. President….Hongera. Dawa pekee ya kumaliza huu mgogoro wa Tembo na Faru, ni kukomesha hiyo biashara na iwe ni kampeni kwa Dunia nzima. Nimefurahi sana alipotoa msimamo wake na wa nchi kwa ujumla kwenye swala la mahusiano ya Jinsia moja. Watanzania tuna mila na tamaduni zetu, hata kama kuna ambazo kumezoea kuiga kutoka kwenye nchi nyingine lakini hili la ushoga, tunalipa na tutaendelea kulipa BIG NOOOOO!!!

    ReplyDelete
  9. JK mwisho!!! Kwa nini Watanzania tusifikirie kumpa 3rd term of service of presidency? Nawasilisha hoja.

    ReplyDelete
  10. Mtoto wa Kabwela,SwedenFebruary 14, 2014

    Hali ya uchumi ni mbaya sana na wanaathirika ni watu wenye kipato kidogo,na ni kweli mawaziri,wabunge na watu wenye madaraka ndio wanaotafuna keki ya Taifa.Rais amejaribu kuzunguka kujibu hilo swali na kudanganya.Ila hawa masikini iko siku watachoka kabisa na mambo ya ajabu sana yatatokea nchini.

    Kuhusu haki za homesexuals, Tanzania na nchi zote masikini ni ngumu kukataa kutowapa haki hilo kundi, kama nchi za Magharibi zikiamua haswa.Historia inajionyesha,nchi za dunia ya Tatu ikiwa Tanzania zilipewa shinikizo na zilikubali mfumo wa vyama vingi na vitu vingi tu. Hata ile Baba wa Taifa hili Nyerere kuwataka WaTanzania kupiga kura ili kupitisha mfumo wa vyama vingi ilikuwa ni viini macho tu.Kama tungekataa tungefutiwa misaada na nchi kama Tanzania haiwezi kujiendesha bila misaada za nchi wafadhili. Asilimia kubwa ya bajeti ya Serikali ni misaada tu.Ona Serikali ilivyoangaika kusafisha image yake mbele ya macho ya wafadhili baada ya habari ya Daily Mail ya Uingereza kuhusu Serikali kushindwa kuwalinda Temabo na Faru wetu.Rais ameangaika kuzindua mabango kabla ya Safari yake ya UK kuhusu kulinda Tembo.Kama nchi tajiri wala isingetishika na habari ile ya Daily Mail ila ufukara wetu ndio tatizo.

    Uganda ilipitisha bill bungeni kuhusu adhabu kubwa kwa Gays lakini Museveni alikataa kusaini na sababu kubwa ni kufutiwa misaada.Kwa hiyo haki za homesexuals zinakuja taratibu tu na Watu wa Magharibi ndio wataamua sio WaTanzania kutokana na nchi ya Tanzania haina nguvu ya uchumi na ni masikini ombaomba.Nacho jaribu kusema kama WaTanzania wanataka kujiamulia mambo Yao wenyewe ni Taifa liwe tajiri.Hamna uhuru wa kuamua pasipo na kuwa na nguvu dhabiti za kiuchumi. Na jana Rais alisema mambo ya udhalilishaji kuhusu gays hajatokei Tanzania kama nchi zingine kwa alikuwa na maana Gays wana ahki kiasi fulani,na hawawezi kudhalilishwa kwa sababu kama nchi wahisani wakijua wanaweza kuondoa misaada Yao.

    Jana JK mmemsikia akiomba kutoka kwa Waamerika kulinda tembo wa Tanzania wakati wao wanalipana mamilioni ya pesa.Ajabu sana Shame on him and all mafisadi.Michuzi naona usibanie comment yangu tafadhali!

    Mtoto wa Kabwela,Sweden

    ReplyDelete
  11. Swali la yule kijana muosha magari amezunguka mbuyu, hakuna jibu alilotoa.

    ReplyDelete

  12. SALUTE JK ON GAY ISSUE!!!

    Eti "civil rights issue of the 21st century"

    Thanks JK, and thanks to all who are against this monster 'gay rights'


    ReplyDelete
  13. Wewe uliyesema third term kichwa chako sio kizuri. Unajua maana ya katiba na sheria ww?? Wewe ni katika vijitu ambavyo tunajaribu kwenda mbele unaturudisha nyuma.

    ReplyDelete
  14. Mtoto wa Kabwela Sweden, nakubalina na wewe. Naona wadau watoa maoni wengine wamepumbazwa kwa kutoelewa ishu. Ni kweli mataifa ya Makubwa yanaamua kila kitu. Wote tunasema JK amekataa ushoga, lakini hapo hapo yupo kwa hao hao jamaa kuomba msaada wa kuwaalinda Tembo. Wenzetu wanasema,usiung'ate mkono unaokulisha.

    ReplyDelete
  15. Gay issue in a shida gain? si watu walivyo. ilimradi hufanyiwi wewe kuna shida gani? waacheni jamani. hata hivyo mambo hayo yapo sana Zanzibar na Pwani kote! tusijidanganye

    ReplyDelete
  16. Kwani kuna shida gani gays wakifanya mambo yao. Huo ni uamuzi wao, Kila mtu anao uamuzi wa kufanya anachopenda kufanya. JK angesema kuwa hatuwezi kuhalalisha ndoa za jinsia moja siyo kusema kwamba kwa Tanzania bado sana. Alichosema kizuri ni kwamba hakuna aliyeuawa kwa kuwa gay.

    ReplyDelete
  17. Wadau na Watanzania wezangu tuwe tunsema ukweli kama ulivyo. Wengi wenu mnashabikia Mkuu kama yuko sahihi, ambapo ukweli wa kupotea Tembo unatuumbua wazi mbele ya dunia. Naomba nikopy na ni paste maoni yangu ya awali kutoka kwenye ile picha ya wazungu, wanaharakati, walioshika picha."Unajua kwetu ukiwa Mmbongo ukisema cha maana unapuuzwa, lakini ukiwa ngozi nyeupe unaheshimiwaa, waache watusemee.Ndiyo maana kuna kamsemo ketu kale, "Nabii apendwi kwao". Fikiria majanga yaliyo sababishwa na watu miaka ya karibuni. Wenzetu wa nchi za huko viongozi wangejiuzulu mara nyingi tu, sababu wameshindwa,ingawa mala nyingine si kosa lao. Ndiyo kuwajhibika, siye tupo pale pale. Tukihesabu idadi ya Tembo walivyokuwa awali na sasa, ni wazi uongozi wote ungeachia ngazi. Kwani ni majanga na aibu. Na kesi ya ndugu zetu Alibino hivo hivo, mpaka Wazungu waliposimamia ilo swala hilo ndiyo ukaona haki za ulinzi wa watu unatendeka". Narudia tena, siye ngozi nyeusi bila kuiingiliwa na wazungu ni lazima Tembo waiishe au tutamalizana kila siku wenyewe kwa wenyewe. Tuache ushabiki wa kinafiki na inabidi tuangalia hali halisi ilivyo. Nasema tena viongozi wetu nao wanatuangusha hawaongozi. Watu kukubalina wengi sio kusema kitu kiko sahihi. Mkuu JK hajajibu kitu leo, mie naona maswali yote ameshindwa. Hii ndiyo nasema imebidi aje kwa Pilato bila kupenda, amejileta mwenyewe. Hajajibu jinsi ghani utajiri wa Kitanzania unagawanywa. Ajajibu analifanyia mipango ghani suala la ushogha kwani linakuja ua lipo. Na suala la Tembo ni wazi kwamba limemshinda. Kwenye mtihani namap D, na D kwa vile amejihamini kuja studio akaonyesha ulimwengu mzima jinsi asivyojua jua kutatua ishu. TZ tunatia huruma, halafu eti, watu wanashangilia.

    ReplyDelete
  18. On poverty alleviation, even the 'super powers' are limping on food stamps...vipi JK amalize njaa TZ!

    The best part was on "civil rights issue". Thank you JK, it is not the time, and there will never be that time.
    Kweli ushoga upo, hatukatai, lakini haituingii akilini eti haki zao ni "Civil rights issue of the 21st century".Kweli ZNZ wapo, and so is in almost ALL parts of TZ. NA PIA DUNIANI KOTE WAPO.

    SUALA NI KWAMBA, SHOGA HAKUBALIKI KWENYE MILA ZETU. NA INABAKI HIVYO!
    TUNAJUA WAPO, HATUWAKUBALI, SIO URITHI KWA WATOTO WETU.

    Halafu last but not least, WASITUZUBAISHE NA TEMBO NA MASHOGA.
    Ulaya inafilisika, Marekani 'food stamps' ni issue, njaa imewafikia. Tuwaulize na wao, VIPI????

    ReplyDelete

  19. Portugal kuna njaa
    Italy kuna njaa
    Greece kuna njaa
    Spain kuna njaa

    Njaa= hali ni ngumu sana

    Marekani watu wanaotegemea FOOD STAMPS wanaongezeka kila kukicha,
    Detroit imefilisika, and so is a HANDFUL of other States following suit on Banktrupcy.
    Marekani ina madeni yamewakaba koo. Nchi iko kwenye hali mbaya sana.

    Uingereza imeishiwa nayo, watu wanao 'commute' yaani wanaokaa mbali na mjini London wanakofanyia kazi wanazidi kupungua, they are not commuting anymore! 26% of MEDIUM CLASS are not commuting, imagine, middle class! Mtu akiondoka nyumbani Jumatatu, harudii tena mpaka IJUMAA! Analala kwenye gari, hali hii inatokana na ugumu wa maisha, mafuta bei imepanda sana.

    Ufaransa pia hali inazidi kuwa ngumu kila kukicha.



    Hili linalojitokeza la eti kuwajali tembo na kupigania haki za mashoga ni zuga tu, wanaficha mapungufu yao.

    WANAFICHA HALI ZAO NGUMU ZINAZOWAKABILI KATIKA HIKI KIPINDI TUNACHOPITA, WAMEISHIWA.

    Huyo "muosha gari" ni imaginary tu. JK kasema
    kweli pale aliposema hata yeye pia mtazamo wake ni huohuo. Maana hali ni hivyo almost DUNIANI KOTE, SOMENI NDUGU ZANGUNI.
    KWELI UGUMU WA MAISHA UPO LAKINI SIO SISI PEKE YETU, HATA HUKO KWAO PIA MAMBO NI HAYA HAYA MSIBABAIKE NA UZURI WA MIJI NA MAJENGO YA HUKO, WANAADHIRIKA.

    ReplyDelete
  20. Kuna kitu kimoja kuhusu ushoga ambacho watu wote mnakifumbia macho. Ushoga unaanzaje? Ni kwa watoto kubakwa na jamii kunyamaza kimya. Anayebaka watoto ni nani? Mnajijua katika historia ya Tanzania ni kesi moja tu ya ubakaji iliyasababisha kifungo cha maisha, wengine wote wanaachiwa ama wanahonga maisha yanaendelea. Sasa msubiri na watu weupe waje wawashinikize kama suala la Tembo ndio mnaanza kusema jamii yetu sijui nini. Hivi mmesha wahi kuwaza mzazi mwenye mtoto shoga anajisikiaje katika jamii? Umuulie mtoto wake umtenge ambaye hali hiyo imesababishwa na mtu mwenye akili timamu? Ukiangalia kwenye kipengele hicho ndio utaelewa. Nisichokubaliana nacho ni kuwafungisha ndoa lakini hazi zao nyingine wapeni. Siku hizi ndio balaa kila kukicha watoto wanabakwa na sioni hatua yoyote kali inayochukuliwa , hilo taifa letu la kesho sijui litakuwaje kwa syle hii. Michuzi naomba sana usiibane hii comment. Kila mtu ajiangalie kama mzazi mwenye mtoto wa aina hiyo ndio ataelewa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...