Na Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma. 
 Kamishna Msaidizi wa Polisi Suzan Kaganda  ametoa vitenge 15 kwa ajili ya sare ya kikundi cha ngoma cha Kijiji cha Mlanga Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma na kutoa fedha tasilimu Tshs. 100,000/= kwa ajili ya kuanzisha mradi wa ufugaji wa kuku. 
Ametoa vitu hivyo alipotembelea kikundi hicho ambacho pia kinajishughulisha na ulinzi shirikishi kijijini hapo na kuwaambia kuwa swala la maendeleo ni swala mtambuko hivyo amewataka kuweza kujishughulisha na ufugaji hasa wa kuku kwani wameonekana kuwa na soko Mkoani Dodoma.
Kamishna msaidizi wa Polisi Suzan Kaganda akikabidhi 
fedha taslimu 100,000/- kwa ajili ya mradi wa kufuga kuku katika  
Kijiji cha Mlanga Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma.
Kamishna msaidizi wa polisi Suzan Kaganda akikabidhi vitenge 15 kwa kikundi cha ngoma cha kijiji cha Mlanga Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma watakavyoshona kwa ajili ya sare ya kikundi hicho
Kamishna msaidizi wa polisi Suzan Kaganda akiongea 
na watoto katika kijiji cha Mlanga Wilayani Kongwa Dodoma
Kamishna msaidizi wa polisi Suzan Kaganda  katika  picha ya pamoja na kikundi cha ngoma cha akina mama kijijini Mlanga Wilayani Kongwa Dodoma
Mkuu wa kikundi hicho cha akina mama cha ngoma ktk kijiji cha Mlanga akipeana mkono na Kamishna msadizi wa Polisi Suzan Kaganda baada ya kupokea fedha za mradi wa kufuga kuku..

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...