Katibu Mkuu wizara ya Maendeleo ya Jamii Anna Maembe akizungumza na wataalamu wa wilaya ya Kalambo Mkoa wa Rukwa jana. Kushoto ni Mkuu wa wilaya Moshi Chang'a na kulia ni Kaimu Mkurugenzi Herbert Bilia.

DC wa Kalambo Mkoani Rukwa Moshi Chang'a akikabidhi hundi ya shilingi milioni 7 kwa Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya hiyo Herbert Bilia. Kulia ni Katibu Mkuu wazara ya Meanedeleo ya Jamii aliyetoa hundi hiyo.
Mkuu wa wilaya Kalambo Mkoani Rukwa Moshi Chang'a akizungumza wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wizara ya Maendeleo ya Jamii Anna Maembe (katikati) wilayani humo jana. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Herbert Bilia.
Katibu Mkuu Anna Maembe akisalimiana na akina mama wanakikundi cha kutunza Mazingira katika kata ya Matai wilayani Kalambo Mkoani Rukwa jana. PICHA ZOTE NA RAMADHANI JUMA.
KATIBU Mkuu wa wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na watoto Anna Maembe
ametaka vijana vijana nchini kuachana kabisa na biashara ya dawa za kulevya kwani
inawasababishia matatizo makubwa katika maisha yao badala yake wajiunge na
kutengeneza vikundi vya kijasiriamali ili serikali iweze kuwasaidia kujikwamua kimaisha
na kufikia ndoto zao.
Amesema takwimu za hivi karibuni zinaonesha kuwa, zaidi ya vijana 500 wa Kitanzania
wako kizuizini katika nchini tofauti duniani walikokamatwa wakisafirisha dawa hizo, huku
vijana wengine wapatao 100 wakiwa wamehukumiwa kunyongwa nchini China.
Aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na makundi mbalimbali ya kijamii wakati
wa ziara yake katika kata ya Matai wilayani Kalambo Mkoa wa Rukwa jana, ambapo
alisema biashara hiyo inachafua sana jina la Tanzania katika Jumuia ya Kimataifa
kutokana na idadi kubwa ya vijana kujihusisha na biashara hiyo.
Akizungumzia sera ya Jinsia inayotekelezwa na wizara yake, Katibu Mkuu huyo alisema
haina lengo la kuwafanya wanawake kuwatunishia misuli wanaume katika familia bali ni
kuwawezesha wanawake kushiriki katika uzalisha na kukuza kipato cha familia na taifa
kwa ujumla ili kukabiliana na gharama za maisha ambazo zimepanda sana kwa sasa.
Vilevile alitoa wito kwa wazazi kuhakikisha wanatenga muda wa kukaa na kuzungumza
na watoto ili kujua changamoto zinazowakabili ikiwemo unyanyasaji wa kijinsi na
kisaikolojia wanazokumbana nazo na pia kuwapatia haki zao za kimsingi kama elimu,
afya na kusikilizwa kama ambavyo sera ya watoto hapa nchini inavyoelekeza.
Katika kuimarisha vikundi vya wanawake mkoani Rukwa, katibu mkuu Maembe ametoa
shilingi milioni 43 kutoka katika wizara yake, ambapo vikundi kutoka katika Halmashauri
za wilaya ya Nkasi, Kalambo, Sumbawanga Vijijini na Manispaa vitanufaika kwa mtindo
wa wanachama wa vikundi hivyo kupatiwa mikopo kwa ajili ya kutekeleza shughuli zao
za kiuchumi.
I hope I am right. Looking by name na sura naona huyu Katibu Mkuu wizara ya Jamii mama Maembe alishapata kunifundisha somo la Mathematics nikiwa nasoma shule ya sekondari Forodhani miaka hiyo. Very nice Maths teacher. I liked Maths because of the beautiful way she taught. And I ended up using Mathematics biig time in my current job. Big up mama Maembe, it shows hard work and persistence pays. Hukuishia kufundisha tu, ulijiendeleza kusoma na mpaka kufikia hapo. Society ina mengi ya kujifunza ulikopita.
ReplyDelete