Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Ndugu Job Masima kulia akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya kukagua gari aina ya Ashok Leyland iliyotolewa na Wizara yake kwa ajili kuimarisha viteule vya kijeshi vilivyopo Mkoani Rukwa. Katika kukabiliana na changamoto zilizokuwa zinavikabili vitua hivyo Wizara ya ulinzi kupitia kwa Katibu Mkuu huyo imetoa gari, boti na fedha kwa ajili ya kuboresha makazi na miundombinu katika viteule hivyo. Kwa upande mwingine amesema kuwa baadhi ya vifaa vingine vitatoka makao makuu ya jeshi katika kuboresha viteule hivyo. 
Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Ndugu Job Masima kulia akimkabidhi funguo ya gari Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya kama ishara ya makabidhiano ya gari mbili pamoja na michango mingine itakayotumika katika viteule vya jeshi vya Mkoani Rukwa.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akiwasha gari hilo kama ishara ya kupokea misaada hiyo kwa viteule vya Jeshi vilivyopo Mkoani Rukwa.
Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Ndugu Job Masima wa pili kushoto akitoa majumuisho ya ziara yake kwa uongozi wa Mkoa wa Rukwa leo. 
Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu  Symthies Pangisa kushoto  akizungumza katika kikao hicho cha majumuisho ambapo amemshukuru Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na msafara wake kwa kazi nzuri waliyoifanya Mkoani Rukwa katika kipindi chote cha ziara yake ya siku tatu.
Baadhi ya wajumbe walioshiriki kikao hicho cha majumuisho wakifuatilia kwa makini.(Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @Rukwareview.blogspot.com)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...