Master Oscar John

Mimi ni kijana wa kitanzania ambaye nimekulia katika maadili ya kidini na malezi mazuri ya kifamia, napenda nichukue fursa hii nitangaze nafasi ya mchumba ambaye kama ata kidhi vigezo vyangu atakuwa ndio mke wangu wa ndoa. Kifupi mi ni mtaalam wa IT naishi Dar es salaam. 
Mchumba ninaye mtaka ni vema awe amekulia malezi ya kidini kwa sababu mimi ni mcha Mungu na napenda kusali kwa hiyo napenda na yeye awe hivyo, malezi yangu ni ya dini ya kikristo ni vema na yeye akawa huko ila itakapobidi anaweza akatoka dini tofauti na mimi, ila itamlazimu aamie kwenye dini yangu, napenda pia asiwe zaidi ya miaka 24, kwa upande wa elimu asiwe chini ya kidato cha nne. 
Namtanguliza Mungu mbele kwa yeyote ambaye anaona anafaa katika vigezo vyangu ili ambariki kabla hajafanya mawasiliano na mimi. 
Kwa mawasiliano na mimi: 
Mungu akutangulie wewe utakayeona 
unafaa kuishi na mimi kama mke na mume. 

Asanteni na karibu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Kila la heri, dogo. Nimependa ukweli wako. Hukuficha kitu - umeweka picha, email address, simu... Unaonekana mtu serious. Nakuombea ajitokeze mtu serious pia.

    ReplyDelete
  2. Mdau umeshakosea priciple moja muhimu katika ndoa nayo ni COMPROMISE !
    Yaani unataka mtu abadili DINI jee wewe uko tayari kubadili ?

    ReplyDelete
  3. Kumekucha. Mungu atutetee. Sijui nisemaje.

    ReplyDelete
  4. Sasa kama wewe ni mcha Mungu si umwombe Mungu akupatie mchumba? Mchumba unakuja tafuta kwenye Mtandao? Mungu akuinulie Nuru ya uso wake na kukuongoza. Amen.
    Rev. MsemaKweli.

    ReplyDelete
  5. Kijana wa watu anatia huruma. Yaani kukulia kote kwenye maadili ameshindwa kupata mwenye maadili mwenzake alipokulia au anaogopa kuwatokea wadada. Kwa vile hajataja anaka kabila gani ngoja waje kutoka kishimundu wamuingize mjini na vihandu vyao. Lol!
    Asipate shida watamtongoza sana sura yake inalipa ila wenzake wa kule wanataka awe mhasibu, mwanasheria, mfanyabiabiashara, jambazi maarufu ili waweze kununua makabati ya picha na mbeho.

    ReplyDelete
  6. We kijana, vipi.mtoto wa mjini borne & raised unatafutia mchumba kwenye michuzi blog?something is not smelling right here..

    ReplyDelete
  7. haki ya MUNGU hii dunia sasa? bora zirudi zile enzi za wazazi kutafutia wachumba watoto,au ndio maana siku hizi michango ya harusi mingi,kumbe wanapendana asubuhi mchana ndoa jioni zinavunjika.

    ReplyDelete
  8. Kijana kweli inawezekana una nia ya kuoa kweli lakini nadhani mahali ulipoenda kutafuta mchumba sio waongo wengi sana mjini hapa maisha magumu

    ReplyDelete
  9. Dogo umenisikitisha sana, hivi kwa kweli kabisa na IT yako unatafuta mchumba hapa?umeniangusha sana dogo,na umetuangusha sisi watu wa IT. Kingine hata mchungaji/padri wako akisikia hichi ulicho kifanya hapa lazima akupigishe sala ya TOBA, hakikubaliki kabisaaa,hapa umeenda kimwili zaidi na sio kiroho,so dogo hapa umeleta matamanio ya kimwili sala ya TOBA inahusika, Kwa wazazi wako pia wakisikia hili watasikitika sana,kama kweli wamekulea vizuri na kwa maadili yote hukupaswa fanya hivi,ulitakiwa Ongea na Baba yako na yeye angeitisha kikao cha familia,wajomba zako wangekuja na mashangazi zako na nina kuambia wallah ungepewa kitu cha ukweli,wazee wanafahamu mambo. So dogo naomba fanya ifuatavyo:
    Kwa kutimia blogu hii hii omba radhi kwa wafuatao;
    1. Wazazi/Familia yako
    2. Mchungaji/Padri wako
    3. Walimu wako
    4. Nasisi wanataaluma wenzio wa IT

    Asante.

    ReplyDelete
  10. Anony mtaalam wa IT umeongea jambo la busara na la maana big up. Mdogo wangu umetuangusha sana hata sisi wacha mungu wenzio. Hebu funga kwa kadiri ya taratibu za dhehebu lako na kuongea na mungu juu ya hilo nae anasikia na atakujibu ukiwa kweli u mcha mungu na umelelewa ktk maadili ya dini.

    ReplyDelete
  11. Ni ajabu kwamba watu wa IT wanafikiri kuwa wameangushwa na huyu kijana. Muaibike! Hamjui kwamba mtandaoni ni sehemu ya watu kukutana? Hii si ndio moja ya faida ya teknolojia? Na nyie mnaomsimanga kwa kuwa ameomba mtu mchaji...mlitaka akutane na msichana wapi, kwenye madisko? Ukweli na kwamba japo mtu anaweza kuwa na kazi yenye staha Fulani haimaanishi kuwa atavutiwa na kila msichana anayepita mbele yake. Inawezekana kuwa amejaribu na kushindwa. Mungu atakusaidia kupata mwenza ikiwa mtakutana kanisani, maktaba, shuleni, kazini, kwenye daladala au hata mtandaoni! Mungu yupo mahali pote!! Kwani mbona zamani kulikuwa na pen-pals kwenye magazeti? Kijana wa watu amefanya kitu cha heshima katika kuelezea mahitaji yake bila kumtukana mtu yeyote, lakini baadhi yenu mnamsimanga na kumdhihaki. Heshima ni kitu cha bure; at the very least, if you disagree with his approach, say nothing and leave him alone. After all, it is likely you don't know him and this post is not meant for ya!

    Kwako kijana, Mungu akujalie upate yule unayemtafuta na kuishi maisha ya upendo, amani na uchaji.

    ReplyDelete
  12. Ni ajabu kwamba watu wa IT wanafikiri kuwa wameangushwa na huyu kijana...

    person, I find what kind' a good human being' you're. for special advice to a kid.

    Kutokana na maombi alio yaomba, na maelezo alio jielezea.

    mdau holland.

    ReplyDelete
  13. Duuh hongera dogo. Lakini nakupa pole kama kweli wewe ni mtoto wa Dar mjini umekosa mchumba unategemea utapata humu kwenye mtandao pole sana dogo. good luck.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...