Kocha wa mchezo wa masumbwi nchini, Rajabu Mhamila 'Super D' katikati akiwa na baadhi ya mabondia wanaofanya mazoezi katika Klabu ya Uhuru uwanja wa Basket, Kariakoo jijini Dar es Salaam,wakati alipofika na kuwakabidhi baadhi ya vifaa vya mchezo wa Masumbwi.kutoka kushoto ni Athanas Kibwe,Omari Bai, Raymond Mbwago Mussa Sindano na kocha wa Kambo hiyo Mohamed Chipota .
Kocha wa mchezo wa masumbwi nchini, Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akikabidhi vifaa vya mchezo wa masumbwi zikiwemo Gloves pamoja na DVD za mafunzo ya mchezo huo kwa Kocha wa Klabu ya Uhuru uwanja wa Basket, Kariakoo jijii Dar es Salaam,wanaoshuhudia ni baadhi ya mabondia wanaofanya mazoezi kwenye kambi hiyo.

-------------------------------
KOCHA wa mchezo wa masumbwi nchini,Rajabu Mhamila 'Super D' ameipiga tafu  Klabu ya mchezo wa ngumi ya Uhuru uwanja wa Basket, Kariakoo Dar es salaam kwa kuwapati vifaa vya mchezo huo.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo,Super D alisema amevutiwa na uanzishwaji wa Klabu hiyo ambayo ina uwezo mkubwa wa kuwatoa mabondia wazuri kipindi kijacho.

 "Mimi nimeamua kujitolea Gloves za mikono mitatu kwa kuanzia ili wapate moyo wa kuendelea na mazoezi pamoja na DVD za mafunzo ya mchezo wa masumbwi,maana ndio timu ambazo tunazitegemea kwa siku za usoni kutuletea mabondia wakali watakaoweza kutuletea medali na kuipatia sifa nchi hii".

Akizungumza mara baada ya kupokea vifaa hivyo,Kocha wa Klabu ya Uhuru uwanja wa Basket, Kariakoo,Mohamed Chipota amesema vifaa hivi pamoja na DVD za mafunzo ya ngumi zimekuja wakati muhafaka kwa kuwa walikuwa na uhaba wa vifaa kama hivyo.

"Hivyo tunaomba wadau mbalimbali wajitokeze kutupa sapoti kama alivyofanya Super D yeye ni kocha wa Mkoa wa Kimichezo Ilala sasa hapa kama amewekeza mabondia wa ilala sasa watatokea hapa kwa siku za usoni.

"Tumeanza hivi karibuni lakini mategemeo yangu ni kuibua vipaji vipya kabisa vya mchezo wa masumbwi nchini",alisema Chipota .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...